Bismillahir Rahmanir Rahim

 

UNION OF MADRASSAHS IN DODOMA (UMADO)

 

Back Home UMADO  /  Qardhul Hasanah  /  Fomu Ya Maombi Ya Mkopo

MUONGOZO YA MAOMBI YA MKOPO

Bismillahir Rahmanir Rahim

UMOJA WA MADRASSAH - DODOMA

µ  U M A D O  µ

P.O. Box 2736 - DODOMA, TANZANIA

 

ZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ

 

MAOMBI YA MKOPO (QARDHUL HASANAH) KWA WALIMU WA UMADO

  

MUONGOZO YA MAOMBI YA MKOPO

 

1.    Huu mkopo usiyo na riba (mkopo mzuri) QARDHUL HASANAH ni kwa ajili ya:

 

         a)      Walimu wa Madrassah zilizosajiliwa na UMADO tu.

         b)      Ni maalum kwa walimu ambao wamesajiliwa na UMADO.

         c)      Walimu wanaofanya kazi ya kufindisha Madrassah wakati wote.

 

2.   Mkopo utatolewa kwa vikundi vya walimu watano na siyo kwa mtu binafsi.

 

3.   Kiwango cha juu cha Mkopo ni Tshs. 250,000/= kwa kikundi, sawa na Tshs. 50,000/= kwa kila              mtu.

 

4.   Mkopo wote urejeshwe ukiwa kamili ndani ya wiki 12,  huu ni muda wa mwisho, sawa na kurejesha T.shs. 4,200/= kwa kila mtu,  au Tshs. 21,000/= kwa kikundi kwa idadi ya watu 5  (4,200/= x 5 ) au T.Shs. 252,000/= kwa wiki 12 (4,200/= x watu 5 x wk 12 ).  Kiasi kilichoongezeka cha Ths. 2,000/= zitakuwa gharama za uendeshaji hasa  uchapishaji.

 

5.   Urudishaji wa mkopo utakuwa wa kila wiki wa siku ya Jumamosi. Marejesho yatawakilishwa na mkuu wa kikundi. Atatakiwa kurejesha T.sh. 21,000/=  kila Jumamosi hadi pale kiasi cha fedha za mkopo zitakaporejeshwa zote.

 

6.    Kundi lote litawajibika kulipa kwa kiwango sawa, Mungu aepushe, iwapo miongoni mwao mtu ameshindwa kulipa deni linalohitajiwa.

 

7.    Fomu ya maombi ya mkopo inapatikana kwa kulipia T.sh. 2,000/= kwa kila mtu.

 

8.    Kujaza na kuwakilisha fomu ya mkopo hakutakuwa na maana ya kuwa umepata mkopo (utapata mkopo).

 

9.   Mwisho wa uhakiki wa fomu  utatolewa na Kamati ya Mkopo ambao uamuzi wao utatakuwa wa mwisho.

 

10.  Pindi fomu zikihakikiwa, kila mtu atahitajika kulipa Tsh. 4,000/= kama gharama za uendeshaji sawa na Tsh. 20,000/= kwa kikundi cha watu watano.  Gharama hizo zilipwe kabla ya kupewa mkopo.

 

11.  Fomu za maombi ziambatanishwe na:

a)   Mchanganuo wa Mradi wa biashara ambao mtu au kikundi wanaotaka kufanya.

b)   Barua ya dhamana kutoka kwa Imam wa Msikiti unaoswali daima.

c)   Barua ya dhamana kutoka kwa Balozi wa nyumba kumi.

d)   Hati ya dhamana kwa vitu visivyo hamishika mfano kiwanja, shamba, nyumba   kama dhamana thabiti.

12. Mungu aepushe iwapo mtu yeyote katika kikundi atashindwa kurudisha mkopo uliotakiwa, watu wengine katika kundi hilo watawajibika kutakiwa kurejesha mkopo kwa niaba ya mkosaji.

 

13.  Iwapo kundi zima limeshindwa kurejesha mkopo uliotakiwa hatua zozote katika hizi zinaweza kuchukuliwa. 

a)      Kuwakilisha malalamiko kwa Imam wa Masjid kisha kwa Balozi wa nyumba Kumi.

b)      Kuwakilisha malalamiko katika kituo cha polisi kilichoko karibu.

c)      Kupeleka malalamiko mahakamani.

d)      Kuuzwa kwa mali  zisizohamishika kufidia gharama za mkopo.

14.  Kundi  litakaloweza kutunza sheria (masharti) na kurudisha mkopo kwa muda unaotakiwa watastahili kupewa mkopo kwa mara ya pili.  Kwa kiwango kikubwa cha zaidi ya Tshs. 350,000/=.

 

15.  Kundi litakaloshindwa kurudisha mkopo kwa muda ulipoangwa au kushindwa kutimiza masharti yoyote ya mkopo halitapewa, mkopo wowote na UMADO au Msaada kwa yeyote.

 

16.  Kabla ya kutoa mikopo, UMADO itaandaa Semina kwa ajili ya kuwaelemisha wahusika jinsi ya uendeshaji wa biashara, utunzani wa mahesabu pamoja na kutuzarekodi.  Semina hiyo itakuwa ni muhimu kurudiwa kwa wale watakao hakikishiwa kupewa mkopo.

 

 

 

Back Home UMADO  /  Qardhul Hasanah  /  Fomu Ya Maombi Ya Mkopo