Bismillahir Rahmanir Rahim

 

Welcome to

Union of Madrassahs in Dodoma
(UMADO)

 

Back Home  /  UMADO  /  Know more about UMADO

MUUNDO WA MTIHANI WA QURAN NGAZI YA MAS’HAF

Utangulizi:

Mtihani wa Quran katika ngazi ya Mas’haf utakuwa katika sehemu nne (4). Jumla kuu ni Alama 100.

Sehemu A: KUSOMA KWA KUANGALIA KITABU - (ALAMA 30)

Msimamizi atampa mwanafunzi kitabu kusoma kutoka kwenye Mas’haf kwenye maeneo mawili (2) tofauti. Mwanafunzi atasoma katika sehemu zote mbili si chini ya mistari kumi (10).

Msimamizi atamtahini mwanafunzi katika maeneo yafuatayo na kumpa alama kama ifuatavyo:

A) Tartiil: Usomaji kwa sauti nzuri na ya kupendeza. (Alama 5 x 2 = 10)

B) Tajweed: Kuangalia sheria za Tajweed kwa mfano: Idgham, Idh-har, Nun Tanween, Shadda, Madda, Makhraji, n.k. (Alama 5 x 2 = 10)

C) Fasaha: Kusoma bila kusita au kusimama, na mfululizo ndani ya ayah. (Alama 5 x 2 = 10).

Sehemu B: KUSOMA KWA KUHIFADHI - (ALAMA 30)

Wanafunzi wanatakiwa kusoma kwa hifadhi sura kamili yeyote mawili (2) katika sura zifuatazo:

1) Al-Qariah     2) Al-Adiyah     3) Zilzaal     4) Al-Bayyinah     5) Al-Qadr

6) Al-Alaq     7) At-Tiin     8) Alam Nashrah     9) Ad-Dhuhaa     10) Al-Layl

Msimamizi ataangalia kwenye maeneo yafuatayo kama ilivyo katika Sehemu (A) na kufuata katika utaratibu wa kutoa alama sawa kwa Sura zote mbili, kwa mfano:

A) Tartiil (Alama 5 x Sura 2 = Alama 10)

B) Tajweed (Alama 5 x Sura 2 = Alama 10)

C) Fasaha (Alama 5 x Sura 2 = Alama 10)

Hivyo kila Sura itakuwa na alama 15 na itakuwa : [ Sura 2 x Alama 15 = Jumla Alama 30 ].

Sehemu C : TAFSIR KWA KISWAHILI - (ALAMA 20)

Mwahafunzi atahitajika kutafsiri katika Kiswahili kutoka katika Sura 2 tu zozote zifuatazo:

1) Al-Falaq     2) An-Naas     3) Lahab     4) Ikhlaasi     5) Kafiruun

6) An-Nasr     7) Ma’uun     8) Kawthar     9) Fiil     10) Quraish

Sehemu D : FUNDISHO AU UJUMBE KUTOKA KATIKA SURA - (ALAMA 20)

Mwanafunzi atatakiwa na kuwakilisha ujumbe mafundisho mawili (2) kutoka sehemu yeyote katika sura mbili kutoka sura zote 10 zilizochaguliwa kama zilivyo orodheshwa sehemu C.

Kila ujumbe utakuwa na alama 5, hivyo : [ Mafundisho 2 x Sura 2 x Alama 5 = Alama 20 ]

N.B. (Zingatia):

  • Mtihani itafanyika katika tarehe zifuatazo, Insha Allah: Jumamosi 04/12/2004 - Mtihani wa Quran, Ngazi ya Juzu. Jumapili 05/12/2002 - Mtihani wa Quran, Ngazi ya Mas’hafu.
  • Walimu wanaombwa kuwatayarisha wanafunzi wao kwa mitihani na kuwatia moyo kwa wanafunzi wote washiriki katika mitihani.
  • Wanafunzi watakaofaulu mtihani kama wale watakao pata alama juu ya 50% watapewa VYETI pamoja na ZAWADI, Insha Allah.
  • Walimu watakao shiriki katika mitihani watapewa posho na zawadi.

Nashukuru kwa ushirikiano. Wa Billahi Tawfeeq.

 

 

Back Home  /  UMADO  /  Know more about UMADO