Bismillahir Rahmanir Rahim

 

Welcome to

Union of Madrassahs in Dodoma
(UMADO)

 

Back Home  /  UMADO  /  Know more about UMADO

MUUNDO WA MTIHANI WA QURAN "JUZUU AMMA"

UTANGULIZI:

1. Muundo wa Mtihani wa Quran "Juzu ya Amma" utakuwa katika ngazi kuu 2, ambazo ni:

    a) Juzu AMMA kabla ya AL-HAMDU     b) Juzu AMMA kuanzia AL-HAMDU.

2. Kila ngazi itakuwa na mtindo wake wa kutahini pamoja na mgawanyo wake wa "marks".

(A) JUZU AMMA KABLA YA AL-HAMDU

1. Kutambua herufi moja moja zikiwa zimechanganywa:

    Mfano: "Alifu" kisha "Nun" halafu "Yee" kisha "Swadi".

    MARKS: 1 kila herufi. Ataulizwa mtahiniwa herufi 10 tu. Jumla ya "marks" zitakuwa 10.

10 Marks

2. Kuzitambua herufi zikiwa kwenye maneno yenye alphabet 4 hadi 6.

    Mfano:

    Herufi 5 zitatakiwa kutambuliwa. Kila herufi ina alama 2. Jumla katika sehemu hii ni 10.

10 Marks

3. Kusoma maneno ya silabi tatu au nne.

   Mfano:

   Maneno 5 yataulizwa. Kila neno ‘Alama’ 2. Jumla Alama 10.

10 Marks

4. Kuandika herufi kama zinavyotajwa na msimamizi wa mtihani.

    Zitatajwa herufi 10. Kila herufi itakuwa na alama 1. Jumla katika sehemu hii itakuwa na alama 10.

10 Marks

5. Kubaini herufi katika kurasa zozote zile za juzu AMMA kabla ya kufikia AL-HAMDU.

    Zitaulizwa herufi 10 tu. Kila moja itakuwa na alama 1. Jumla sehemu hii itakuwa na Alama 10.

10 Marks

(B) JUZU AMMA KUANZIA AL-HAMDU

1. Sura zitakazotahiniwa ni pamoja na:

    a) TAFSIRI NA MAF’HUM.

1- Surat Qul Huwallahu.

2- Surat Idhaa Jaa’a.

3- Surat Inna Anzalnaahu.

4- Surat Al-hamdu.

5- Surat Alamtara

    Kila sura, mtahiniwa atatakiwa kutoa maf’hum ya ujumla. Kufanya hivyo ni Alama 3, kwa kila sura.

15 Marks

b) KUSOMA KWA KUANGALIA.

 i) Surat Al-Hamdu.

    ii) Surat Alamtara.        

    iii) Surat Inna Anzalnahu

    iv) Surat Araita.

    v) Surat Qul Huwallahu.

    Kila mshiriki atatakiwa kusoma kwa kuangalia. Alama ni 3 kwa kila sura.

15 Marks

c) KUSOMA GHAIBU / HIFDH

i) Surat Al-hamdu

ii) Surat Alamtara

iii) Surat Inna Anzalnahu

iv) Surat Ara’aita

v) Surat Qul Huwallahu

   Kila mwanafunzi atatakiwa kusoma Ghaibu (hifdhi). Kila Sura ina alama 4.

20 Marks

JUMLA 100 Marks

WABILLAHI AT-TAWFIIQ

 

 

Back Home  /  UMADO  /  Know more about UMADO