Uongozi wa Umoja Wa Madrassah
Dodoma (UMADO) uliandaa kikao Jumamosi tarehe 07/05/2005 ambacho
madhumuni yake kilikuwa ni kukutana na walimu wote wa Madrassah juu ya
kufanikisha mashindano ya Quran Tukufu kila mwaka. Yafuatayo ndiyo yaliyokubalika
katika kikao na yameaanza kufanyiwa kazi rasmi:
UMUHIMU WA KUHIFADHI
QURAN TUKUFU
Hii ni mashindano ya kusoma
Quran kwa Hifadhi kwa ajili ya vijana wa Madrassah. Zoezi hili ni muhimu
kutokana na hadithi ya Mtume Muhammad (saww) inayosema kuwa: "Hakuna
dhambi kubwa kama mtu kuisoma Quran kisha akaisahau". Kutokana na
hadithi hii, ni lazima kuandaa mikakati ya kudumu kwa vijana wote wa
Madrassah kuhifadhi Quran. Kutokana na umuhimu huu, UMADO imeandaa
mikakati kuwashindanisha vijana wa Madrassah katika kuhifadhi Quran kila
baada ya miezi sita yaani mara mbili kwa mwaka, na hii kupelekea miaka
mitano, mwanafunzi awe amehifadhi mas-hafi yote juzuu thelathini.
HIFADHI:
Walimu wa Madrassah
walipendekeza kuwa
kwa hatua ya kwanza, wanafunzi
watatakiwa kuhifadhi kwa muundo wa mpangiliowa Quran ilivyopangwa
kuanzia Juzu ya 30 na 29.
SIFA ZA VIJANA WA
MADRASSAH KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA QURAN:
- Umri wowote ila mwisho awe
miaka 20.
- Awe mwanafunzi wa Madrassah.
- Madrassah iwe imesajiliwa
na UMADO.
- Awe anajua kuisoma Quran
kwa hifadhi kuanzia juzu ya 30 na 29.
KANUNI ZA MASHINDANO:
-
Msomaji atatakiwa azijue
hukumu zote za Quran Tajweed kwa mfano Idgham, Idh-har, Nun
Tanween, Shadda, Madda, Makhraji, n.k.
-
Asome kwa mfululizo bila ya
kusita.
-
Usomaji kwa sauti nzuri na ya
kupendeza yatakayozingatiwa na majaji.
-
Kuhifadhi kwa msomaji katika
maeneo wa Quran kuanzia juzu ya 30 na 29.
-
Majaji wanaweza kuisoma Aya
au Sura kwa kifupi kisha msomaji aiendeleze.
KUSHIRIKI:
Kila madrassah itatoa
washindi 2 (1 mvulana na 1 msichana). Ikitokea Madrassah haina msichana
wa kushirikisha katika mashindano hayo, basi itabidi uletee wavulana
wawili.
Ushiriki utafanyika kikanda
yaani Madrassah 10 (kumi) zitakuwa kanda moja. Kuna Madrassah 70 na
kanda 7. Kwa hiyo jumla ya kanda saba kutapatikana washiriki 140. Rejea
jedwali ya kila Madrassah na kanda yake hapa chini.
ZAWADI:
Kwa kipindi chote hicho
zawadi kubwa zitatolewa, kwa vitu halisi kama cherehani kwa wasichana,
baiskeli kwa wavulana, kofia, vitambaa vya kichwani, kanzu na fedha
taslimu kadri wafadhili watakavyo changia zoezi hili. Mshindi wa kwanza
kwa wavulana atapata Baiskeli na msichana atapata Cherehani. Mshindi wa
pili na watatu watapata fedha taslimu. Washiriki wote wengine watapewa
zawadi za kushiriki. Aidha na walimu watapewa zawadi zao maalum kutokana
na kazi nzuri ya kulisimamia na kuwatayarisha wanafunzi kushiriki katika
mashindano haya.
WITO:
Kikao kilitoa tamko la pamoja
kuwa zoezi la kuhifadhi Quran litakuwa la kudumu hivyo linahitaji nguvu
za pamoja kwa Waislam wote kushiriki kwa hali na mali. Lengo ni vijana
wetu wahifadhi Quran na kuwa na namba nzuri ya wasomaji wa Quran na
kuweza kuwafanya wawe tayari kushiriki mashindano nchini na nchi za nje.
Asante sana. Wa Billahi
Tawfeeq.