|
1.0 |
UTANGULIZI |
|
1.1 |
Neno la Awali |
|
|
Kwa muda mrefu sasa
taasisi muhimu ya kiislam, taasisi ya “madrasa” imeachwa na kupoteza
hadhi yake. Pamoja na hilo, taasisi hii imeacha pengo kubwa ambalo
halizibiki kwa urahisi ila kwa kuinua hadhi ya Madrasa zetu.
Umma wa Waislam unazidi
kupata kizazi kinachokosa haki za kimsingi za kuandaliwa kama madhalifa.
Mwenyezi Mungu katika Qurani 51:56 ametwueleza “SIKU WAUMBA MAJINI
NA WATU ILA WANIABUDU” ili kutekeleza lengo hilo, waislamu
lazima waipe hadhi Madrasa. Kadhalika ili kufikia hadhi yetu wanaadam
kama inavyoelezwa katika Quran 2:30 waislam lazima tuipe madrasah, hadhi
yake sahihi. Kwa sababu hizo, kuna haja ya kufanya fikra juu ya kuinua
hadhi ya madrasa zetu kwa ajili ya kuuendeleza umma wa kiislam utapotea
na kuacha wanaoitwa Waislam lakini ummah wa kiislam haupo. |
|
|
|
|
1.2 |
Maana ya Madrasa |
|
|
Ilivyozoeleka, madrasa
ni kituo cha kiislam ambapo watu hupata elimu juu ya mambo ya msingi
katika uislam. Wengine wameita Shulel za Quran, wengine wamesema, vyuo
vya Quran, na wengine wanaelewa kuwa madrasa ni vituo vya watoto ambapo
masomo ya Quran, kusoma na kukandika hufundishwa. |
|
|
|
|
1.3 |
Kazi
zinazonasibishwa na Taasisi ya Madrasa |
|
|
Madrasa zetu Tanzania,
kwa muda mrefu tangu Historia ya kuingia kwa uislam nchini
zimenasibishwa na kazi zinazofanywa na taasisi hii. Kwa ujumla madrasa
zetu zimejikita katika taaluma zifuatazo:-
(i)
Kuandika herfu za kiarabu.
(ii)
Kuzisoma herfu za kiarabu.
(iii)
Kutafsiri llugha ya kiarabu.
(iv)
Kusoma Quran kwa ghaibu au kwa kutazamia.
(v)
Jinsi ya kufanya ibada maalum na kanuni zake.
Mfano, ibada, swala, swaum, hija na utoaji zakat na sadakat.
|
|
1.4 |
Athari za Madrasa
kujikita katika shughuli hizo |
|
|
Kwa kuwa Madrasa ni
vituo vya elimu ya kiislam, na kwa vile madrasa zinaoa elimu hizo tu,
basi elimu ya kiislam inafahamika kuwa ni ile tu inayohusiana na:
-
Kusoma na kuandika Quran.
-
Kukariri sura za Quran na tafsiri zake.
-
Kanuni za utekelezaji wa nguzo tano.
-
Kukariri hadithi kadhaa za Mtume (s.a.w).
-
Kukariri visa vilivyo katikak lugha ya kiarabu.
|
|
|
Matokeo ya hilo, Uislam
nao umeeleweka kukwa ni mambo ya kimaisha yanayohusiana na shughuli hizo
tu. Nje ya shughuli hizo si vitu vya lazima katika uislam. Mfano
kuksimamisha dola ya kiislam.
|
|
2.0 |
HISTORIA YA ELIMU YA
MADRASA TANZANIA KWA UFUPI |
|
|
Ø
Historia ya Elimu ya Madrasa
Tanzania inanasibiana na Historia ya kuenea kwa uislam katika Afrika
Mashariki kuanzia Pwani hadi bara.
Ø
Elimu itolewayo na Madrasa zetu ilichipuka
tangu wakati walivyoanza kuja Waarabu kutoka Saudia, Oman, Uajemi,
Hadhramaut na Yemen.
Ø
Karne ya 9 na 10 wahamiaji kutoka Saudia
walianza kusihi BENADIR (Pwani ya Somalia).
Ø
Karne ya 12 Waarabu wageni (Afro-arabs)
walianza kufika hadi mji wa Kilwa.
Ø
Karne ya 12 wageni kutoka Hadhramawt na
Yemen waliingia Afrika Mashariki. Wageni hawa nao pia walitoa
elimu inayohusu uislam. Lakini kufahamu uzito wa elimu waliyoitoa
kunategemea ufahamu wa sababu zilizowaleta Afrika Mashariki. Hawakuja
kueneza uislam na kuufundisha uislam. Bali wali kuja kutokana na:
(i)
Njaa iliiyokuwapo Arabuni wakati huo.
(ii)
Ukame huko Arabuni.
(iii)
Ukandamizaji wa Kisiasa uliotawala huko.
|
|
|
|
|
2.1 |
Kustawi kwa Elimu ya
Madrasa Afrika Mashariki |
|
|
Ø
Mwaka 1332, Mwarabu aitwaye IBN BATUTA
alipotembelea Kilwa alikuta mji umekaliwa waliokuwa wakitumia lugha ya
Kiswahili.
Ø
Baadaye miji ya Tanga, Dar-es-Salaam,
Mombasa, Lamu, Malindi, na Mikindani vikawa vituo vya kueneza
uislam na elimu ya kiislam katika miji ya Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwandda, Zaire, Msumbiji, Malawi na Burundi. |
|
|
|
|
2.2 |
Maarifa yaliyotolewa na njia za kufundishia |
|
|
Ø
Maarifa yaliyotolewa na kuonekana hayo
ndiyo maarifa ya uislam ni pamoja na:
(i)
Zipi ni nguzo za imani na maana yake.
(ii)
Zipi nguzo za Swala na maana yake.
(iii)
Namna ya kusoma Quran, lugha ya kiarabu na vira
kadhaa.
(iv)
Sirah ya Mtume (s.a.w)
(v)
Kanuni zinazotawalal utendaji wa Ibada Maalumu. |
|
|
|
|
|
Ø
Maarifa haya yalifundishwa kwa njia kuu ya
Kipurure. Mwanafunzi hakusoma kwa kuwa mdadisi sana. Wanafunzi
walikasirishwa waliyofundishwa.
Ø
Walimu wa kufundisha hayo, ni wale tu,
walioonekana wanaweza kuyasoma hayo. Hakukuwa na mazingatio kuhusu
uwezo na ujuzi wa mfundishaji kufikisha maarifa anayoyatoa.
Ø
Kwa sababu hizo, pia njia kuu ya kudhibiti
nidhamu, ilibaki kuwa ni viboko tu.
Ø
Kwa ujumla taaluma kuu za elimu ya Madrasa
zilizotawala ni KUSOMA, KUANDIKA, KUIFADHI na KUIGA ambazo
zilitolewa na walioweza kuzipata taaluma hizo. |
|
|
|
|
2.3 |
Dosari za Elimu ya
Madrasa iliyotolewa wakati wa Waarabu |
|
|
·
Utangulizi |
|
|
Ø
Dosari hizo zimetokana na asili ya kuenea
kwa dini na elimu ya Kiislam Afrika Mashariki, hususan Tanzania.
Ø
Tatizo linakuja kwa vile Uislam na elimuk
ya Kiisam:-
(i)
Vilenea katika taratyibu za walioeneza
kkujitafutia maisha yao wala si kwa madhumini ya kufanya
umisionari.
(ii)
Vilienezwa na wailam ambapo hawakuwa na
maandilizi ya kufanya hivyo hivyo hakukuwa na matayarisho yoyote ya
malengo ya kieleimu.
Ø
Matokeo yake uislam ulifundishwa ili
kupata wenzi na washirika katika mas[ala ya kijamii kama vile:
o
Misiba
o
Harusi n.k.. |
|
|
|
|
|
·
Utangulizi |
|
|
(i)
Zilifundishwa Taaluma chache tu.
Mfano: Kusoma, Kuandika, Kukariri Quran.
Taaluma hizo si pana kiasi cha kuwawezesha wanafunzi kuuhani uislam
kifikra, au vyovyote Taaluma hizo hazimwezeshi mwanafunzi kumudu
changamoto zinazoibuka kila kukicha; Japo uislam haushindwi na
changamoto yoyote ile.
(ii) Njia
za kuendeleza nidhamu, na maadili zilikuwa viboko tu, ukali tu, pasi na
kuchunguza tatizo kwa lengo la kkuondoa tatizo hilo na kusaidia.
(iii) Njia
za kkufundishia hazikuzingatia umuhimu wa kuendeleza na kuhusisha nyanja
tatu za kujifunza.
(a)
Nyanja ya ung’amuzi (Cognitive domain).
(b)
Nyanja ya matendo (Psychomotoar domain)
(c)
Nyanja ya kuhusisha (Affective domain)
Kila nyanza hapo inaumuhimu katikak uislam wa mtu mmoja mmoja au jamii
na hatimaye Ummah.
(iv) Hakukuwapo
chombo maalum cha kijamii, kinachosimamia swala zima la utoaji wa Elimu
hii. Matokeo yake kila mmoja alifundisha kadiri na namna alivyodhani ni
sawa.
|
|
|
|
|
2.4 |
Athari za dosari
hizo |
|
|
(i) Kukosekana kwa
taaluma muhimu za kifiqih |
|
|
Mfano:
-
Taaluma inayowezesha kkuhusianisha mazingira na
fatwa kadhaa za kifiqih.
-
Taaluma inayofafanua hukumu kadhaa za kifiqih na
yanayotokea katika maisha. Katika hili, kumekosekana taaluma ya
kubainisha tofauti ya RIRA na HIBA. |
|
|
|
|
|
(ii) Watu wachache sana
ndio waliweza kwendelea na elimu ya Madrasa kwa
kiwango cha juu
kwa kulinganisha na waislam wengine. |
|
|
Mfano:
Ni Masheikh wachache
waliweza kkufikia kiwango Fulani. Matokeo hata vitu vidogo vidogo
kuweza kufahamika kwa waislam wote, vinafahamika na masheikh tu. |
|
|
|
|
|
(iii) Kuibuka kwa
Matabaka miongoni mwa waislam kutokana na dosari hizo,
kumeibuka
matabaka kadhaa mingoni mwa waislam. |
|
|
Mfano:
o
Tabaka la wasomi wa elimu katika mfumo huu
wa madrasa tu.
o
Tbaka la waliosoma elimu ya madrasa kidogi
na elimu ya kisekula kidogo.
o
Tabaka la waliosoma kiasi elimu ya
kisekula na kukosa elimu ya madrasa lakini badaye (ukubwani) wakajifunza
elimu ya uislam kwa mfumo mwingine.
Mahusiano ya matabaka
haya hayasaidii kuendeleza uislam na waislam wa kiislam, ni sumu kwa
maendeleo ya jamii ya kiislam. |
|
|
|
|
3.0 |
MATATIZO
YANAYOIKABILI ELIMU YA MADRASA TANZANIA |
|
|
(i) Utangulizi |
|
|
Taasisi ya Madrasah
inazidi kukpoteza hata hadhi yake ndogo iliyokuwa nayo. |
|
|
Mfano:
Jamii haiipi hadi na
thamani stahiki licha ya kuwa madrasa ni taasisi muhimu katika
kurithisha mila, na mfumo mzima wa uislam toka kizazi hadi kingine.
Wazazi wa watoto wa kiislam leo hii hawana hari ya kupeleka watoto wao
kwenye vituo vya madrasa. Wala wazazi hao hawana hata haja ya kujua
mikati ya madrasa zinazowazunguka. |
|
|
|
|
|
(ii) Matatizo |
|
|
Matatizo yanayoikabili
elimu ya madrasa ni: |
|
|
|
|
3.1 |
Matatizo ya
Kitaasisi (Institutional Problems) |
|
|
(a) Hakuna mfumo wa
uendeshaji elimu ya madrasa. Mfumo huo |
|
|
Mfumo huo hautoi picha
halisi juu ya nani hasa ndiye mratibu au msimamizi wa elimu ya Madrasa.
Kwa sababu hiyo hakuna upimaji wala tathimini yoyote ili kuelewa mustak
bal wa elimu hii muhimu |
|
|
|
|
|
(b) Kukosekana kwa
“usare” (uniformity) katika ufundisjaji. |
|
|
Matokeo yake anapohama
motto kwenda madrasa nyingine anaathirika kitaaluma. |
|
|
|
|
|
(c) Hakuna utaratibu
fasaha/muafaka wa kuwahusisha wazazi wa Kiislam katika kujadili
maendeleo na kutathimini uendeshaji wa madrasa. Athari yake ni wazazi
kutojihusisha na uendelezaji wa madrasa zetu na ufuatiliaji wa taaluma
muhimu zipatikanazo. |
|
|
|
|
|
(d) Kukosekana kwa
utaratibu wa kubadilishana mawazo baina ya walimu tofauti tofauti, juu
ya uboreshaji wa njia za ufundishaji na mafanikio katika uendeshaji
madrasa. |
|
|
|
|
|
(e) Kukosekana kwa
mipango inayohusiana na madrasa, wanafunzi na walimu. Athari yake ni
kupungua kwa idadi ya wanafunzi na walimu wa madrasa. |
|
|
|
|
|
(f) Kukosekana kwa
utaratibu maalumu juu ya vigezo vinavyomuwezesha mtu kuwa mwalimu. Kwa
kawaida yeyote anayejua kusoma na kuandika herufi za kiarabu, kusoma
Quran na mambo kadhaa katika Ibada maalumu za kifiqih, aweza kuwa
mwalimu hata kama sifa za kitabia, na uwezo wa kkurithisha elimu kwake
ni vikwazo. |
|
|
|
|
|
TANBIH:
Aina za walimu zaweza
kkuwa kama ifuatavyo:-
(i)
Mwenye sifa (Qualified) – Anazo sifa kitabia,
anaweza na ujuzi wa kkufundisha na ana elimu.
(ii)
Mwenye sifa (Underqualified) – Anayo elimu ila
hana mbunu bora za ufundishaji.
(iii)
Asiye na sifa (Unqualified) – Hana sifa hata
kidogo. Huyu ni hatari sana. |
|
|
|
|
|
Matatizo ya Kijamii |
|
|
(a) Fikra za watu
juu ya elimu ya madrasa na thamani yake |
|
|
-
Jamii na mtu mmoja mmoja wanachukulia elimu ya
msingi ya madrasa ni kusoma Quran na kujua kanuni muhimu za utekelezaji
wa Ibada maalumu kama vile Swala, hija, swala ya maiti, kushona
sanda na kadhalika.
-
Athari yake ni kuwa, mara baada ya watoto kufikia
ngazi hiyo huonekana imetosha na kwamba, wana elimu ya kutosha juu ya
uislam. Elimu kuhusu uislam inapungua miongoni mwa waislam. |
|
|
|
|
|
(b) Uchumi duni kwa
wazazi na walimu |
|
|
- Umaskini
na kipato kidogo kwa walimu wa madrasa inakuwa tatizo kubwa kwa
uendeshaji wa madrasa zetu. Hali hii husababisha walimu wa madrasa
kutenga muda kidogo sana kwa ajili ya kazi ya madrasa. Kadhalika
kujituma juu ya kuboresha madrasa hupungua.
-
Vile vile pato la wazazi kuwa dogo huchangia
tatizo. Mara nyingi watu wenyekipato cha chini ndio wanaopeleka watoto
wetu madrasa na wenye uwezo na wito wa kiislam wao huwaajiri walimu wa
kuwafundisha watoto nyumbani. Kwa sababu hiyo, wazazi wengi hawana
uwezo wa kkuchangia fedha muhimu kwa ajili ya madrasa. Wakati mwingine
mchango wao huwa kidogo na mgumu kupatikana.
-
Athari ya hayo, ni kudorora kwa madrasa zetu na
kupatikana kwa watoto, mabarabara, vijana wasio na elimu sahihi ya
msingi kuhusu uislam na hatimaye kuporomoka kwa maadili. |
|
|
|
|
|
(c) Mfumo wa elimu
ya nchi na utaratibu wa kisekula |
|
|
Mfumo wa elimu ya
kisekula umembana kiasi motto anayesoma madrasa kutokana na utaratibu
ulivyo. Uendeshaji wa elimu ya kisekula umezaa desturi ya “Tuition” (masomo
ya ziada), desturi amabyao sit u inamfanya motto achoke bali pia
inamkosesha muda wa kuhudhuria katika madrasa zetu. |
|
|
Mfano:
- Mtoto wa darasa la
kwanza na pili wanaingia shule kwa zamu, mara asubuhi, mara saa tano,
mara mchana. Hii inaleta ugumu kwa madrasa kuratibu jinsi ya kuwasaidia
watoto.
- Mtoto wa darasa la
kwanza atokapo shule, anapumzika kidogi, kasha anaenda “Tuition” masomo
ya zaida.
- Mtoto wa darasa la
tano hadi saba, anakosa muda kabisa. Muda wote, kutwa mzima
anashughulishwa na elimu ya kisekula na usiku anajisomea nyumbani.
|
|
|
Athari ya tatizo hili
ni kushuka kwa mahudhurio ya watoto katika madrasa zetu, na mara
nyingine kuwapo kwa mahudhuria yasiyotabirika na kuelezeka. Mara kuna
mahudhurio ya kuridhisha mara mabaya. |
|
|
|
|
|
(d) Shughuli za
Kijamii miongoni mwa Waislam |
|
|
-
Ndani ya jamii ya Kiislam, inapotokea shughuli
kama vile harusi na kadhalika, madrasah nyingi kuhusishwa. Mfano
kuandaa kaswida kwa ajili ya maulidi harusini. Hili hupunguza za muda
wa ufundishaji na kujifunza katika madrasa zetu.
-
Athari yake ni kuongezeka kwa tatizo katika
madrasa zetu. Wazizi wengine huona kua hakuna haja ya watoto kusoma
madrasa hizo. |
|
|
|
|
4.0 |
SOLUHISHO KWA
MADRASA ZETU |
|
4.1 |
Utangulizi |
|
|
-
Ni vigumu kuliondoa tatizo hili kwa kulifanya
jukumu hilo kuwa la watu Fulani tu. Mfano, kulifanya liwe jukumu
la masheikh tu, au jukumu la walimu tu, au la wazazi tu. Inapaswa kuwa
ni tatizo linalomgusa kihisia kila muislam.
- Kwa
hakika elimu hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya uislam na
waislam kiitikadi, kitaaluma, kielimu n.k. |
|
|
|
|
4.2 |
Mfumo |
|
|
- Kunahaja
ya kuudhurusi mfumo wa elimu ya madrasa na kuangalia namna ya
kuuendeleza na kuuboreha kwa manufaaa ya kikazi cha kiislam.
- Mfumo
wa madrasa zetu uendane kabisa na haja iliyopo katika jamii kwa lengo la
kuwaendeleza watoto kitaaluma. |
|
|
|
|
4.3 |
Walimu |
|
|
- Kuwepo na mpango
maalumu wa kuwaendeleza walimu kielimu, kitaaluma na kiuchumi ili
kuwaongezea hari ya kujituma na kukfikiri kwa ajili ya maendeleo ya
taasisi hii muhimu, “madrasati”. |
|
|
Mfano:
Kuwepo kwa warsha,
makongamano na semina ili kuwawezesha walimu kushirikiana ujuzi na mbinu
za kufundishia na kuendeshea madrasa zetu. |
|
|
|
|
|
-
Walimu wawe wabunifu kiuchumi ili waweze
kujikwamua kiuchumi na kuendeleza madrasa zetu.
-
Walimu wasijione kuwa wao ni waislam au watu wa
daraja la chini sana kimaisha. Bali wajione wao ni watu muhimu
na kazi yao ni jukumu lao si jukumu la mtu Fulani na wala hawafanyi kazi
hiyo ili tu kuwaridhisha watu Fulani bali ili kumridhisha allah (s.w).
|
|
4.4 |
Jamii ya Kiislam |
|
|
- Ifanye
fikra juu ya jinsi ya kuboresha na kuendeleza madrasa zetu na watoto
wetu katika taaluma muhimu za kiislam.
-
Jamii nzima ieleweshwe juu ya nafasi sahihi ya
Madrasa na Elimu ya Madrasa kwa maisha yua Waislam nchini. |
|
|
|
|
4.5 |
Taasisi za Kiislam |
|
|
Zishirikiane kuona
jinsi ya kutatua matatizo hayo. |
|
|
|
|
5.0 |
TAALUMA MUHIMU KWA
WALIMU WA MADRASA |
|
5.1 |
Utangulizi |
|
|
Kila nyanja inahitaji
taaluma Fulani ili kuifanya nyanja hiyo iwe makini na yenye manufaa
kwamaisha na ummah kwa ujumla. Hata mitume (radhi za Allah ziwafikie)
walipewa taaluma maalumu kwa kazi zao. Katika maisha yetu tunahitaji
taaluma zinazowezesha watu kutekeleza majukumu yao katika mazingira
wanayoishi. |
|
|
Mfano:
Mwalimu wa madrasa
anahitaji taaluma juu ya;
(i)
Uendeshaji wa madrasa.
(ii)
Ufundishaji.
(iii)
Saikolojia ya watoto na malezi.
(iv)
Taaluma inazofundisha kama vile Fiqih,
Tareikh, Qurani, Kiarabu, Tawhiid, Sirah, Akhlaq n.k. |
|
5.2 |
Njia za kkufundishia
(Muhtasari) |
|
|
Zipo njia kadhaa Bwana
Mtume (s.a.w) amekuwa akizitumia katika kufundishia watu. Pia Quran
imeeleza njia kadhaa kwa ajili ya ufundishaji na uchamasishaji. Kwa
muhtasari njia hzo ni pamoja na zifuatazo. |
|
|
|
|
|
(a) Simulizi
(Narration) |
|
|
-
Hii ni njia ambayo mwalimu anafundisha kwa
kutumia visa vya kubuni au visa halisi. Njia hii inafaa sana
kutumika hususan kwa watoto wadogo.
-
Katika Quran njia hii imetumika kutafundisha mara
kadhaa. Kanuni na njia yenyewe katika Quran zimeelezwa katika “NJIA ZA
KUFUNDISHIA KATIKA MADRASA ZETU”. Hapa ni muhtasari tu.
-
Njia hii yaweza kutumika katika kufundisha Sira
ya Mtume, Akhlaq, Tareikh, Fiqih hata tawhiid. Alimradi mwalimu afahamu
jinsi ya kuitumia njia hiyo kwa ufanisi. |
|
|
|
|
|
(b) Uelezeaji
(Description) |
|
|
- Njia hii hutumika
kuelezea dhana au wazo Fulani katika uislam. Muhimu kwa mwalimu ni
kuifahamu misingi ya njia hii pamoja na kuelewa mazingira yanayofaa kwa
njia hii. |
|
|
Mfano:
(i)
Ili kutoa maf’hum nzuri kuhusu “UISLAM” kama dini njia hii yafaa
kutumika.
(ii)
Ili kufunldisha vizuri, mazingira ya vita vya Badr, Uhud, Khandaq
n.k. kwa lengo la kkufundisha mazingatio yanayopatikana, mwalimu aweza
kutumia njia ya UELEZEAJI (Description) |
|
|
- Kadhalika, cha muhimu
ni maarifa kuhusu njia hii. |
|
|
|
|
|
(c) Njia ya
Uoneshaji (Demonstration) |
|
|
- Ni njia inayotumika
kufundishia mada zinazolenga kutoa ujuzi kwa wanafunzi kutenda matendo
maalum: |
|
|
Mfano:
(i)
Swala la mait.
(ii)
Swala la Faradh na Sunnah.
(iii)
Kushona Sanda.
(iv)
Kuosha Maiti.
(v)
Kuchukua Udhu n.k. |
|
|
-
Mada kama hizi zikifundishwa pasipokutumia njia
hizi, ueleo wa wanafunzi unaathirika.
-
Mwalimu anatakiwa kuifahamu njia hii kwa
madhumuni ya kuitumia kwa ufanisi. |
|
|
|
|
|
(d) Njia ya ugunduzi
na udadisi |
|
|
- Njia hii inamtaka
mwalimu aoneshe tatizo kasha aongeze wanafunzi katika kugundua suluhisho.
Kwa kufanya hivi, milki ya ung’amuzi (Cognitive Facult) itakuwa
imeendelezwa. Quran inasisitiza matumizi ya milki ya ung’amuzi
(Cognition domain). |
|
|
Mfano:
(i)
Baada ya kufundisha “Tawhid” – Mwalimu anaweza
kutoa habari ya kweli kuhusiana na tawhiid kasha wanafunzi wakajadili
kwa mnasaba wa tawhid.
(ii)
Mwalimu aweza kufundisha “Tareikh” – Hijar kutoka
Makka kwenda Madina, alafu wanafunzi watatakiwa kugundua wanachojifunza.
(iii)
Mwalimu awezatoa tatizo liliopo katika jamii kwa
mnasaba wa uislam, kasha akawataka wanafunzi waonyeshe sabbu na
suluhisho. |
|
|
|
|
|
(e) Njia ya
Kuhidadhi |
|
|
- Hii ni muhimu sna
katika elimu na maarifa ya kiislam. Mwalimu anatakiwa kuwawezesha
wanafunzi kuhifadhi katika mada kadhaa. |
|
|
Mfano:
(i)
Ktika Swala, mwalimu atumie njia rahisi kwa
wanafunzi kuhifadhi.
(ii)
Katika Wudhuu, mwalimu atumie njia hii pia ili
wnafunzi waweze kuhifadhi maneno muhimu.
(iii)
Katika Dua, wanafunzi wahifadhishwe dua.
(iv) Katika
Tarekh, wanafunzi wahifadhishwe aya na hadithi mbalimbali
zinazonasibiana na matukio katika mada. Mathalani, kufundisha Mkataba
wa hudaybiya, Quran 48:1. 48:18 ni vema zikahifhadhiwa. Pia katika
kufundisha AKHLAQ mwalimu awahifadhishe watoto, Sura ya 64.4 ikiwekana,
kulingana na umri wa watoto, Pia wahifadhi Quran 33:21. |
|
|
|
|
|
(f) Njia za
Kufundisha Quran |
|
|
Njia na mbinu pamoja na
mikakati ni muhimu sana katika ufundishaji wa usomaji Quran, vinginevyo
motto atosoma muda mrefu sana ili kuelewa. Baadhi ya mbinu za
kufundishia ni pamoja na kusoma herufi bila irobu kwa njia ya ubao, kadi,
daftari n.k. |
|
|
MUHIMU:
-
Mwalimu afundishe kwanza herfu bila irabu.
Yaani: ALIF, BE …….
-
Kisha afundishe Irabu. Yaani: FAT’HA,
KISRA, ……
-
Afundishe kuchanganya herufi hizo na rabu;
Mfano: BE FAT’HABA, TE FAT’HATA …….
-
Mwalimu atumie michezo kadhaa kwa watoto
kuzitambua herufi.
Mfano: NGAZINGAZI, KIKAPU, UPANGAJI, GURUDUMU ZA GARI, NYUMBA
…. n.k.
-
Mwalimu afundishe kuchanganya SILABI ili kupata
neno. Ni vizuri Mwalimu akaanza na kinachoeleweka kwenda kisichoeleweka.
Mfano: Kumwezesha motto kuandika BABA kwa herufi za Kiarabu,
kasha aandike neno la kiarabu kwa herfu hizo. |
|
|
|
|
6.0 |
HITIMISHO |
|
|
Mwalimu anapaswa sit u
kujua anachokifundisha, bali pia kufahamu na kuweza kutumia njia na
mbinu muafaka. Kwa kawaida hatupaswi kulenga kusema sana, au kueleza
mengi, bali tulenge kuwezesha mengi kufahamika kwa urahisi zaidi. |
|
|
|
|
7.0 |
MWISHO |
|