TANZANIA MUSLIM STUDENTS ASSOCIATION

[TAMSA]

 

                                       MOROGORO

 

 

WARSHA YA VIONGOZI  WA  MATAWI

 

 

 

 

 

 

UONGOZI WA TAASISI NA JUMUIYA ZA KIISLAMU

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

IMETAYARISHWA NA:

 

MKOA WA MOROGORO.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

(MU)

 

 


 

BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIM

TANZANIA MUSLIM STUDENTS ASSOCIATION

 

MADA: UONGOZI WA TAASISI NA JUMUIYA ZA KIISLAM

MADHUMUNI: (OBJECTIVES)

Kuwawezesha washiriki kuwa na mwelekeo, uelewa na stadi muhimu katika kutekeleza jukumu lao. Kufikiwa hili maudhui inafafanuliwa kwa kutumia mifano halisi sambamba na kuwa na kazi katika makundi.

 

MATARAJIO (EXPRECTATIONS)

Inatarajiwa kuwa washiriki wataweza:

(i)                  Kufafanua dhana “uongozikama mchakato, fani na sanaa.

(ii)               Kufafanua matumizi stahili ya madaraka ya uongozi.

(iii)             Kufafanua aina ya mahusiano yanayofaa baina ya viongozi na wafuasi  na hatimaye kuwezesha hilo.

(iv)              Kujitathmini kwa kuzingatia dhana ya uongozi, madaraka na uhusiano baina ya viongozi na wafuasi

STADI: (SKILLS)

Stadi zifuatazo zinalengwa.

(i)                  Uelewa sahihi kuhusu uongozi.

(ii)               Namna bora ya kuwezesha wafuasi wamkubali kiongozi na uongozi wake.

IKISIRI (ABSTRACT)

“….. waulizeni wanojua kama hamjui” (22:41)

 

 Ili kutekeleza maelezo ya ayah hii, kuna haja ya kuwa na mazingira yanayowezesha kubadilishana uzoefu. Warsha na semina ni miongoni mwa mazingira hayo. Katika mada hii dhana ya uongozi imeelezwa. Mengine yaliyoelezwa ni dhima ya uongozi, madaraka ya uongozi, misingi ya maadili ya uongozi, madaraka ya uongozi, misingi ya maadili ya uongozi, wasifu wa kiongozi wa kiislamu, pamoja  na  uhusiano baina ya viongozi na wafuasi. Hoja katika mada hii ni kwamba ufanisi wa kiongozi unategemea sana matumizi ya madaraka, maadili ya kiongozi, na wasifu wake kiongozi.

 

 

 

 

 

 

 

1.0 UTANGULIZI

Uongozi wowote ni sanaa ya kushughulikia  masuala ya watu na

kushawishi mwenendo wa mwanadamu, na kuuongoza mwenendo

huo kuelekea shabaha maalum, kw namna ambayo itawezesha

 kupatikana utii katika hilo, kuwa na imani na hilo na zaidi

ya yote, heshima kutokana na kufanya hivyo” (Fathi Yakan- Tasfsiri)[1]

 

Kufanikiwa kwa kiongozi katika dhamira yake, kunategemea sana sifa na uwezo alionao. Hata hivyo hatupaswi kusahau kuwa kuna vipawa vya asili alivyonavyo kiongozi, vinavyompa uwezo wa kufanikiwa katika uongozi, lakini si kwa kiasi kikubwa sana, Haiba (Personality) ya kiongozi hujazilizwa na sifa  nyingine kama vile zile za kiitikadi, kiroho, kiumbile, kiutawala kimaadili na wasifu wa mwenendo wa mtu.

 

Nafasi ya kiongozi, mtindo na mchakato wa uongozi ni muhimu, nyeti na tete katika harakati zozote zile. Kama kiongozi hana sifa zinazotakiwa, na kama mtindo na mchakato wa uongozi haufai kimsingi na kiutendaji, hakuna shaka kwamba harakati za taasisi husika zitadorora na kupooza kama sio kifo cha Jumuiya na taasisi hiyo.

 

2.0 MASUALA YA MSINGI

Hakuna mashaka kwamba taasisi zetu za kiislam ikiwemo TAMSA, zinaongozwa na viongozi, hivyo kwa sababu uongozi ni jambo la msingi, inafahamika kuwa katika uislam uongozi ni amanah na jukumu ambalo linapaswa kufanywa kwa uwezo mzuri wa kiongozi. Katika maudhui ya mada hii, masuala yafuatayo yanaguswa:-

 

1.      Kwamba kila mmoja ni mchunga, suala linakuwa “ Je kila mtu ni kiongozi miongoni mwa wanajumuiya? Je kama ndivyo hivyo nani miongoni mwa wanajumuiya anapaswa kutiiwa kwanza?

2.      Kwamba uongozi ni sanaa, ni mchakato na ni fani: Je uelewa huu unanasibiana na mfumo, kanuni na utendaji wa uongozi wa TAMSA?

3.      Kwamba uongozi ni dhamana, ni amanah na ni dhima : Je viongozi wa TAMSA hususan matawini, wanafanyaje katika kuzingatia kuwa uongozi ni  dhamana, ni amanah na ni dhima? Ni mimi wasifu wa kiongozi ambaye uongozi wake ni dhamana, ni amanah na ni dhima .

4.      Kwamba ili kutekeleza jukumu la Uonozi, kiongozi anahitaji madaraka: Je viongozi wa TAMSA watumieje madaraka ili kufanikiwa kupata ufanisi?

5.      Kuna namna fulani ya uhusiano wa kiutawala  baina ya viongozi na wafuasi , suala ni kuwa, hivi namna ya uhusiano wa kiutawala baina ya viongozi wa TAMSA na baina ya viongozi kwa ujumla na wanaoongozwa inawezesha ufanisi?

 

3.0 MFUMO WA DHANA

“….. Waulizeni wanaojua kama ninyi  hamjui” (Q. 22:41)

 

Waislamu tumewekewa mfumo na utaratibu mzuri kimaisha katika kila kipngele. Katika mfumo wa kijamii waislam tunatakiwa kuwauliza wanaojua ikiwa hatujui. Bila shaka warsha hii ni mazingira ya kutekeleza mafundisho ya aya hii. Katika kufanya hivyo tuanangalia dhana za uongozi kama zilivyoelezwa na wanachuoni kadha.

 

3.1 Maana ya Uongozi

Uongozi ni mchakato ambao kwao, kiongozi anatfuta ushiriki wa wafuasi kwa hiyari yao, katika jitihada za kuyaelendea malengo fulani.[2] Aidha tuanweza pia kusema kwamba uongozi ni mchakato wa kuwaelekeza watu na kuwashawishi katika utendaji pasipo kutumia mabavu.[3]

 

Kwa kuzingtia sifa na nafasi ya kiongozi katika mafanikio ya taasisi, asasi, Jumuiya au kikundi ama harakati, ni rahisi kuona kuwa uongozi si tu ni mchakato, bali pia  ni sanaa, ni ujuzi na  uongozi ni fani. Kwa kifupi fasili zifuatazo zinatoa uelewa kuhusu Uongozi.

 

(i)                  Uongozi ni sanaa kwa vile unahitaji uzuri na kupendeza katika mikabala (approaches). Unahusu ustadi wa kiongozi katika kuwashawishi na kuwalekeza watu.

Hakuna kulazimishana katika dini” (Q. 2:256)

 

Aya hii inatuonyesha dhahiri kuwa kiongozi anapaswa kuwa na uwezo wa kubuni na kuyaweka maono katika vitendo vya wafuasi katika mtindo wa kushawishi. Uwezo huu ni snaa. Kwa hiyo utaalamu, umahiri na umilisi unahitajika.

 

(ii)               Uongozi ni mchakato kwa kuwa unahitaji kupitia hatua na ngazi kadhaa katika kushwishi na kupata ushiriki wa wafuasi. Kwa sababu hiyo kuongoza siyo kushawishi mara moja na kusubiri matokeo ya ushawishi.

(iii)             Uongozi ni fani maalum kwa kuwa zipo kanuni, ipo misingi na yapo maadili maalum. Kwa kufuata na kuzingatia kanuni na misingi ya uongozi wa kiislamu kama inavyoelezwa katika Quran na Sunnah, mtu atafanikiwa katika matumizi ya fani hii ya uongozi.

(iv)              Uongozi ni kundi la watu wanaozindua na kuwAtumikia wafuasi, kwa kuonyesha njia na mwelekeo kIsha kuwashawishi wafuasi wafuate njia hiyo.

(v)                 Uongozi ni utaratibu uliopo wa kutumia sanaa katika mchakato wa kuwawezesha watu kufika katika malengo yaliyowekwa.

 

3.2 Haja na nafasi ya uongozi katika Jumuiya na Taasisi

Kwa kuzingatia fasili   ya uongozi, iwe mchakato, sanaa au fani na hata kundi la watu, ni rahisi kueleza haja ya uongozi  na kueleweka. Katika mafundisho ya uislam, uongozi si suala la hiyari, bali ni suala la lazima. Kila wawapo wawili au zaidi, uislamu umeelekeza kuwa lazima  awepo kiongozi. Hii maana yake ni kuwa kila penye watu, uongozi ni lazima. Suala litabaki juu ya aina ya uongozi.

Katika kutekeleza mafundisho ya uislamu kuhusu uongozi, viongozi wanapaswa kukumbuka kuwa:-

(i)                  Uongozi ni dhamana

(ii)               Uongozi ni dhima

(iii)             Uongozi ni amanah.

 

Pamoja na hayo, kutokuwa na uongozi ni kujikaribisha kwa shaitwan.

                         Al- hadith

Kila mmoja wenu ni mchunga na kila mcunga ataulizwa

 juu ya kile alichokichunga” [4]

 

Tukiitafakari hadithi hii kwa kina , tunajifunza kuwa pamoja na kuwa na uongozi, wanaoongozwa pia, wanalo jukumu la kuhakiisha kuwa hakuna uongozi mbovu watu wajue kuwa wataulizwa juu ya walichokidhunga.   Iwapo ummah, Jumuiya, taasisi au asasi itakuwa na uongozi mbovu, kila mwanjumuiya atakuwa mas’ulia.

 

3.3 Dhima ya Uongozi

Dkt. Jamal Badawi, profesa na mwenyeit wa menejiment na stratejia, katia Chuo kiku cha Nevada, alisema kwmba katika uislam dhima mbili za uongozi katika uislamu ni:-

 

 

 

(i)                  Utumishi kwa anaowaongoza.

Kwanza, kiongozi ni mtumishi wa anaowaongoza (sayyid al qawan khadimuhum) anapaswa kuwatafutia ustawi bora na kuwaongoza katika mema.[5] Dhana kwmba kiongozi ni mtumishi wa anaowaongoza ni sehemu ya uislamu tangu kwanza kwa uislamu. Kiongozi anayezingatia dhima hii anachukua nafasi ya utumishi kwanza. Suala la muhimu kujiuliza, ni kwa kiwango gain kiongozi  wa taasisi,  jumuiyah na Harakati za Kiislamu wanajiuliza kuhusu dhamira yao ya utumishi au ni viongozi pasiopo dhamira hii ya utumishi. Tukumbuke kuwa “mkuu wa ummah ndiye khadimu wao”[6]

 

(ii)               Ulinzi wa wafuasi dhidi ya ukandamizaji

Dhima hii nayo imesisitizwa na mtume (s.a.w). kwamba  kiongozi anapaswa kuwalinda wafuasi wake dhidi ya ukatili uonezi na ukandamizaji vile vile kiongozi anapaswa kuwezesha umaizi kuhusu Mungu , taq’wa na haki.[7]

 

(iii)             Ulezi wa wafuasi

Dhima nyingine  muhimu ni ulezi. Ukiwa kiongozi unailea jumuiya, unawalea wafuasi, unailea  taasisi, unailea asasi. Jukumu la ulezi ni muhimu sana katika jamii. Mara zote kiongozi unapaswa kuwaza namna ya kuifanya Jumuiya yako ikue, ikomae, ifanikiwe, itosheke, iridhike, iendelee, ijiimarishe and kujijenga katika maisha ya ki- taasisi pamoja na kufanikiwa katika madhumuni yake. Kwa maelezo hayo, iwe kiongozi ni mlezi, mlinzi au mtumishi bila shaka atahitaji madaraka. Uislamu unayatambua madaraka ya kiongozi.

 

4.0 MADARAKA YA KIONGOZI

Dhana ya madaraka katika muktadha huu ni uwezo wa kupanga, kuratibu, tumia rasilimali watu, taarifa au habari, na fedha,   kufanya mambo ya jumuiya, taasisi au asasi, yaene kama inavyotakiwa.[8] Kama kiongozi atakosa uwezo huu, atadorora na  jumuiya, jamii, ummah au taasisi anayoiongoza itakuwa duavu (inactive). Kuna namna nyingi za kueleza madaraka kwa kuzingatia sunnah and Quran.

 

4.1 Madaraka kutokana na wadhifa (Legistrate power)

Madaraka aliyonayo mtu kutokna na wadhifa katika taasisi. Kwa ujumla uislam haupendekezi waislam kuwa na uamilifu wa kampeni ya kuwatafuta nafasi ya mamlaka. Kwa muislam kufanya kampeni ili apate wadhifa ambao utampa kampeni ili apate wadhifa ambao utampa madaraka, ni ishara ya kuwa mtu huyo anatamaa ya wadhifa kwa maslahi yake binafsi.

                          Al- hadith

“ Usiombe uongozi kwa sababu utakapopewa  uongozi

kutokana na kuomba, utaachiwa pekee yako (bila msaada

 wa Allah kutekeleza jukumu na wajibu unaonasibiana nao)

Na kama umepewa uongozi bila kuomba, utasaidiwa

 (Na Allah katika utekelezaji wa majukumu yako).[9]

 

4.2 Madaraka kutokana na uwezo wa kuzawadia.

Kiongozi ambaye anatawala rasilimali za ummah, jamii au taasisi, anaweza pia kuwa na uwezo wa kuzawadia kutokana na mamlaka na wajibu wkae. Maelezo  haya ni sahihi pia katika mafundisho ya uislam.[10] Inapendeza kusikia kuwa Seyyid na Umar Ibn Khatb[11] (r.q) alikuw aakiwalipa mishahara ya juu, maadisa wa dola ya kiislam. Alifanya hivyo ili kuhakikisha kuwa hawashawishiki kupokea rushwa. Kwa kuwajali aliwateua kama ilivyostahiki, Seyyidna Umar (r.a) akawa kiongozi mashuhuri na aliyefanikiwa. Na kwa namna hiyo, Seyyidna Umar (r.a) ni mfano wa kuigwa na watawala katika ulimwengu leo na pia ni mfano wa kuigwa na  watawala katika ulimwengu leo na pia ni mfano wa kuigwa na viongozi wa jumuiya ya taasisi za kiislam.  Matumizi sahihi ya madaraka haya yanawezeshs mafanikio na uamilifu wa Jumuiya  na taasisi au asasi za kiislamu.

 

Matumizi sahihi ya madaraka haya yanawezesha mafanikio na uamilifu wa jumuiya na taasisi au asasi za kiislamu

 

4.3 Madaraka ya kinguvu (Coeraive power)

Kwa kuwa na mamlaka  ya  kiuonogzi, kiongozi  anao uwezo wa kuadhibu kwa niaba ya anaowaongoza na pia kwa maslahi ya anaowaongoza. Uislamu unatambua kuswihi kwa madaraka haya, lakini unafundisha kuwa madaraka haya yasitumike kuwafanya wafuasi kufanya uovu. Ni kwa ukweli huu Mtume (s.a.w) anayesema kuwa “ Utii (kwa kiongozi) unatakiwa kwa lile tu lililo jema.[12] Katika kusisitiza dhima ya kiongozi wa kiislam na matumizi mazuri ya madaraka ya kinguvu, seyydina Umar (r.a) alinukuliwa akiwaambia watu:

 

Nimekuteulieni magavana na mawakala, siyo kuwaadhibu au

kuchukua fedha zetu bali kuwfundisha na kuwatumika. [13]

 

4.4 Madaraka kwa utaalamu (Expart power)

Kwa kawaida kiongozi mwenye uelewa, maarfia, ujuzi na habari au taarifa muhimu, anayo madaraka kitaalamu. Anao uwezo wa kuwafanya wafuasi watekeleze jukumu fulani kwa mpangilio mzuri na kwa namna sahihi pasipo vikwazo.

Mfano:-

Katika swala ya Jumaa mtu anapaswa kuchaguliwa kuwaongoza wanaosali, kwa kigezo cha ujuzi na maarifa yake juu ya swala. Kutokana na utaalam alionao imam, maamuma watamfuata katika utartibu mzima wa swala. Uwezo huu alionao Imam katika wafanya maamuma wafuate ni madaraka kwa utaalamu juu ya swala.

 

Mfano mwingine ni juu ya uweo wa Amir wa Da’awah kuwafanya wanajumuiya kufuata maelezo yake kutokana na hakika kuwa Amir huyo anayo maarifa juu ya hilo.

 

5.0  MISINGI YA MAADILI YA UONGOZI WA KIISLAM

Kwa sababu kuongoza ni kutekeleza maamrisho ya Allah(s.w) na mafundisho ya mutume (s.a.w) na kwa kuwa kuongoza pia ni kufanya ibada, basi kiongozi anapaswa kutekeleza  majukumu na wjaibu wa maelekezo ya Quran  na Sunnah pamoja na kujikita katika Akhlaq ya kiislam (Islamic Moral character). Akhlaq ya Kiislam inakuwa madhubuti kadiri mja anavyoongeza uthabiti katika kumuamini Mwenyezi Mungu kupitia hatua nne za kiroho.

5.1  Iman

Ni kuamini kwa dhati juu ya kuwa mwenyezi Mungu ni momoja ( Tawhid). Kwa kuwa na Imani, kiongozi atajielewa kuwa yeye na vilivyo chini  yake, vinamilikiwa na Allah(S.w). Pia Iman inamkumbusha kiongozi juu ya  akhera na umas’uulia (Accoutability). Kwa hiyo Iman inamkumbusha kiongozi kuwajibika. Katika kukazia hili, Quran imetaja na kuhusianisha Iman na amali njema si chini ya mara 60