|
Bismillahir Rahmanir Rahim
UMOJA WA MADRASSAH - DODOMA
µ
U M A D O
µ
P.O. Box 2736 -
DODOMA, TANZANIA
ZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ
MAOMBI YA MKOPO (QARDHUL HASANAH) KWA WALIMU WA UMADO
MUONGOZO YA MAOMBI YA MKOPO
1. Huu
mkopo usiyo na riba (mkopo mzuri) QARDHUL HASANAH ni kwa ajili
ya:
a)
Walimu wa Madrassah zilizosajiliwa na
UMADO tu.
b)
Ni maalum kwa walimu ambao wamesajiliwa na
UMADO.
c)
Walimu wanaofanya kazi ya kufindisha
Madrassah wakati wote.
2. Mkopo
utatolewa kwa vikundi vya walimu watano na siyo kwa mtu binafsi.
3. Kiwango
cha juu cha Mkopo ni Tshs. 250,000/= kwa kikundi, sawa na
Tshs. 50,000/= kwa kila
mtu.
4. Mkopo
wote urejeshwe ukiwa kamili ndani ya wiki 12, huu ni muda wa
mwisho, sawa na kurejesha T.shs. 4,200/= kwa kila mtu, au
Tshs. 21,000/= kwa kikundi kwa idadi ya watu 5 (4,200/= x 5 ) au
T.Shs. 252,000/= kwa wiki 12 (4,200/= x watu 5 x wk 12 ). Kiasi
kilichoongezeka cha Ths. 2,000/= zitakuwa
gharama za uendeshaji hasa uchapishaji.
5. Urudishaji
wa mkopo utakuwa wa kila wiki wa siku ya Jumamosi. Marejesho
yatawakilishwa na mkuu wa kikundi. Atatakiwa kurejesha T.sh. 21,000/=
kila Jumamosi hadi pale kiasi cha fedha za mkopo zitakaporejeshwa
zote.
6. Kundi
lote litawajibika kulipa kwa kiwango sawa, Mungu aepushe, iwapo miongoni
mwao mtu ameshindwa kulipa deni linalohitajiwa.
7.
Fomu ya maombi ya mkopo inapatikana kwa
kulipia T.sh. 2,000/= kwa kila mtu.
8. Kujaza
na kuwakilisha fomu ya mkopo hakutakuwa na maana ya kuwa umepata
mkopo (utapata mkopo).
9. Mwisho
wa uhakiki wa fomu utatolewa na Kamati ya Mkopo ambao uamuzi wao
utatakuwa wa mwisho.
10. Pindi
fomu zikihakikiwa, kila mtu atahitajika kulipa Tsh. 4,000/=
kama gharama za uendeshaji sawa na Tsh.
20,000/= kwa kikundi cha watu watano. Gharama hizo zilipwe kabla ya
kupewa mkopo.
11. Fomu
za maombi ziambatanishwe na:
a) Mchanganuo
wa Mradi wa biashara ambao mtu au kikundi wanaotaka kufanya.
b)
Barua ya dhamana kutoka kwa Imam wa
Msikiti unaoswali daima.
c) Barua
ya dhamana kutoka kwa Balozi wa nyumba kumi.
d) Hati
ya dhamana kwa vitu visivyo hamishika mfano kiwanja, shamba, nyumba
kama dhamana thabiti.
12. Mungu
aepushe iwapo mtu yeyote katika kikundi atashindwa kurudisha mkopo
uliotakiwa, watu wengine katika kundi hilo watawajibika kutakiwa
kurejesha mkopo kwa niaba ya mkosaji.
13.
Iwapo kundi zima limeshindwa
kurejesha mkopo uliotakiwa hatua zozote katika hizi zinaweza
kuchukuliwa.
a)
Kuwakilisha malalamiko kwa Imam wa Masjid
kisha kwa Balozi wa nyumba Kumi.
b)
Kuwakilisha malalamiko katika kituo cha
polisi kilichoko karibu.
c)
Kupeleka malalamiko mahakamani.
d)
Kuuzwa kwa mali
zisizohamishika kufidia gharama za mkopo.
14.
Kundi
litakaloweza kutunza sheria (masharti) na kurudisha mkopo kwa muda
unaotakiwa watastahili kupewa mkopo kwa mara ya pili. Kwa kiwango
kikubwa cha zaidi ya Tshs. 350,000/=.
15. Kundi
litakaloshindwa kurudisha mkopo kwa muda ulipoangwa au kushindwa
kutimiza masharti yoyote ya mkopo halitapewa, mkopo wowote na UMADO
au Msaada kwa yeyote.
16.
Kabla ya
kutoa mikopo, UMADO itaandaa Semina kwa ajili ya kuwaelemisha wahusika
jinsi ya uendeshaji wa biashara, utunzani wa mahesabu pamoja na
kutuzarekodi. Semina hiyo itakuwa ni muhimu kurudiwa kwa wale
watakao hakikishiwa kupewa mkopo.
|