|
UTANGULIZI:
1. Muundo wa Mtihani wa Quran "Juzu ya Amma" utakuwa katika ngazi kuu
2, ambazo ni:
a) Juzu AMMA kabla ya AL-HAMDU
b) Juzu AMMA kuanzia AL-HAMDU.
2. Kila ngazi itakuwa na mtindo wake wa kutahini pamoja na mgawanyo
wake wa "marks".
(A) JUZU AMMA KABLA YA AL-HAMDU
1. Kutambua herufi moja moja zikiwa zimechanganywa:
Mfano: "Alifu" kisha "Nun" halafu "Yee"
kisha "Swadi".
MARKS: 1 kila herufi. Ataulizwa mtahiniwa
herufi 10 tu. Jumla ya "marks" zitakuwa 10.
10 Marks
2. Kuzitambua herufi zikiwa kwenye maneno yenye alphabet 4 hadi 6.
Mfano:
Herufi 5 zitatakiwa kutambuliwa. Kila herufi ina
alama 2. Jumla katika sehemu hii ni 10.
10 Marks
3. Kusoma maneno ya silabi tatu au nne.
Mfano:
Maneno 5 yataulizwa. Kila neno ‘Alama’ 2. Jumla Alama
10.
10 Marks
4. Kuandika herufi kama zinavyotajwa na msimamizi wa mtihani.
Zitatajwa herufi 10. Kila herufi itakuwa na alama
1. Jumla katika sehemu hii itakuwa na alama 10.
10 Marks
5. Kubaini herufi katika kurasa zozote zile za juzu AMMA kabla ya
kufikia AL-HAMDU.
Zitaulizwa herufi 10 tu. Kila moja itakuwa na
alama 1. Jumla sehemu hii itakuwa na Alama 10.
10 Marks
(B) JUZU AMMA KUANZIA AL-HAMDU
1. Sura zitakazotahiniwa ni pamoja na:
a) TAFSIRI NA MAF’HUM.
1- Surat Qul Huwallahu.
2- Surat Idhaa Jaa’a.
3- Surat Inna Anzalnaahu.
4- Surat Al-hamdu.
5- Surat Alamtara
Kila sura, mtahiniwa atatakiwa kutoa maf’hum ya
ujumla. Kufanya hivyo ni Alama 3, kwa kila sura.
15 Marks
b) KUSOMA KWA KUANGALIA.
i) Surat Al-Hamdu.
Kila mshiriki atatakiwa kusoma kwa kuangalia.
Alama ni 3 kwa kila sura.
15 Marks
c) KUSOMA GHAIBU / HIFDH
i) Surat Al-hamdu
ii) Surat Alamtara
iii) Surat Inna Anzalnahu
iv) Surat Ara’aita
v) Surat Qul Huwallahu
Kila mwanafunzi atatakiwa kusoma Ghaibu (hifdhi). Kila
Sura ina alama 4.
20 Marks
JUMLA 100 Marks
WABILLAHI AT-TAWFIIQ |