[TAMSA] MOROGORO WARSHA YA VIONGOZI WA
MATAWI UONGOZI WA TAASISI NA
JUMUIYA ZA KIISLAMU IMETAYARISHWA NA: MKOA WA MOROGORO. (MU)

BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIM
MADA: UONGOZI WA TAASISI NA JUMUIYA ZA
KIISLAM
MADHUMUNI: (OBJECTIVES)
Kuwawezesha
washiriki kuwa na mwelekeo, uelewa na stadi muhimu katika kutekeleza jukumu
lao. Kufikiwa hili maudhui inafafanuliwa kwa kutumia mifano halisi sambamba na
kuwa na kazi katika makundi.
MATARAJIO (EXPRECTATIONS)
Inatarajiwa
kuwa washiriki wataweza:
(i)
Kufafanua dhana uongozi
(ii)
Kufafanua matumizi stahili ya madaraka ya
uongozi.
(iii)
Kufafanua aina ya mahusiano yanayofaa baina ya
viongozi na wafuasi na hatimaye
kuwezesha
(iv)
Kujitathmini kwa kuzingatia dhana ya uongozi,
madaraka na uhusiano baina ya viongozi na wafuasi
STADI: (SKILLS)
Stadi
zifuatazo zinalengwa.
(i)
Uelewa sahihi kuhusu uongozi.
(ii)
Namna bora ya kuwezesha wafuasi wamkubali
kiongozi na uongozi wake.
IKISIRI (ABSTRACT)
..
waulizeni wanojua
1.0 UTANGULIZI
Uongozi wowote ni sanaa ya kushughulikia masuala ya watu na
kushawishi mwenendo wa
mwanadamu, na kuuongoza mwenendo
huo kuelekea shabaha maalum,
kw namna ambayo itawezesha
kupatikana utii katika hilo, kuwa na imani na
ya yote, heshima kutokana na
kufanya hivyo (Fathi
Yakan- Tasfsiri)[1]
Kufanikiwa
kwa kiongozi katika dhamira yake, kunategemea
Nafasi
ya kiongozi, mtindo na mchakato wa uongozi ni muhimu, nyeti na tete katika
harakati zozote zile. Kama kiongozi hana sifa zinazotakiwa, na kama mtindo na
mchakato wa uongozi haufai kimsingi na kiutendaji, hakuna shaka kwamba harakati
za taasisi husika zitadorora na kupooza
2.0 MASUALA YA MSINGI
Hakuna
mashaka kwamba taasisi zetu za kiislam ikiwemo TAMSA, zinaongozwa na viongozi, hivyo kwa sababu uongozi ni jambo
la msingi, inafahamika kuwa katika uislam uongozi ni amanah na jukumu ambalo
linapaswa kufanywa kwa uwezo mzuri wa kiongozi. Katika maudhui ya mada hii,
masuala yafuatayo yanaguswa:-
1.
Kwamba kila
mmoja ni mchunga, suala linakuwa Je kila mtu ni kiongozi miongoni mwa
wanajumuiya? Je kama ndivyo hivyo nani miongoni mwa wanajumuiya anapaswa kutiiwa
kwanza?
2.
Kwamba uongozi
ni sanaa, ni mchakato na ni fani: Je uelewa huu unanasibiana na mfumo, kanuni
na utendaji wa uongozi wa TAMSA?
3.
Kwamba uongozi ni dhamana, ni amanah na ni dhima : Je viongozi wa TAMSA hususan matawini, wanafanyaje
katika kuzingatia kuwa uongozi ni dhamana, ni amanah na ni dhima? Ni
mimi wasifu wa kiongozi ambaye uongozi wake ni dhamana, ni amanah na ni dhima .
4.
Kwamba ili
kutekeleza jukumu la Uonozi, kiongozi anahitaji madaraka: Je viongozi wa TAMSA watumieje madaraka ili kufanikiwa
kupata ufanisi?
5.
Kuna namna fulani ya uhusiano wa
kiutawala baina ya viongozi na wafuasi ,
suala ni kuwa, hivi namna ya uhusiano wa kiutawala baina ya viongozi wa TAMSA na baina ya viongozi kwa ujumla
na wanaoongozwa inawezesha ufanisi?
3.0 MFUMO WA DHANA
.. Waulizeni
wanaojua
Waislamu
tumewekewa mfumo na utaratibu mzuri kimaisha katika kila kipngele. Katika mfumo
wa kijamii waislam tunatakiwa kuwauliza wanaojua ikiwa hatujui. Bila shaka
warsha hii ni mazingira ya kutekeleza mafundisho ya aya hii. Katika kufanya hivyo
tuanangalia dhana za uongozi
3.1 Maana ya Uongozi
Uongozi
ni mchakato ambao kwao, kiongozi anatfuta ushiriki wa wafuasi kwa hiyari
Kwa
kuzingtia sifa na nafasi ya kiongozi katika mafanikio ya taasisi, asasi,
Jumuiya au kikundi ama harakati, ni rahisi kuona kuwa uongozi si tu ni mchakato,
bali pia ni sanaa, ni ujuzi na uongozi ni fani. Kwa kifupi fasili zifuatazo
zinatoa uelewa kuhusu Uongozi.
(i)
Uongozi
ni sanaa kwa vile unahitaji uzuri na kupendeza katika mikabala
(approaches). Unahusu ustadi wa kiongozi katika kuwashawishi na kuwalekeza
watu.
Hakuna
kulazimishana katika dini (Q. 2:256)
Aya
hii inatuonyesha dhahiri kuwa kiongozi anapaswa kuwa na uwezo wa kubuni na
kuyaweka maono katika vitendo vya wafuasi katika mtindo wa kushawishi. Uwezo
huu ni snaa. Kwa hiyo utaalamu, umahiri na umilisi unahitajika.
(ii)
Uongozi
ni mchakato kwa kuwa unahitaji kupitia hatua na ngazi
kadhaa katika kushwishi na kupata ushiriki wa wafuasi. Kwa sababu hiyo kuongoza
siyo kushawishi mara moja na kusubiri matokeo ya ushawishi.
(iii)
Uongozi
ni fani maalum kwa kuwa zipo kanuni, ipo misingi na yapo maadili
maalum. Kwa kufuata na kuzingatia kanuni na misingi ya uongozi wa kiislamu
(iv)
Uongozi
ni kundi la watu wanaozindua na kuwAtumikia wafuasi, kwa
kuonyesha njia na mwelekeo kIsha kuwashawishi wafuasi wafuate njia hiyo.
(v)
Uongozi ni utaratibu uliopo wa kutumia sanaa katika
mchakato wa kuwawezesha watu kufika katika malengo yaliyowekwa.
3.2 Haja na nafasi ya uongozi katika Jumuiya
na Taasisi
Kwa
kuzingatia fasili ya uongozi, iwe
mchakato, sanaa au fani na hata kundi la watu, ni rahisi kueleza haja ya
uongozi na kueleweka. Katika mafundisho
ya uislam, uongozi si suala la hiyari, bali ni suala la lazima. Kila wawapo
wawili au zaidi, uislamu umeelekeza kuwa lazima
awepo kiongozi. Hii maana yake ni kuwa kila penye watu, uongozi ni
lazima. Suala litabaki juu ya aina ya uongozi.
Katika
kutekeleza mafundisho ya uislamu kuhusu uongozi, viongozi wanapaswa kukumbuka
kuwa:-
(i)
Uongozi ni dhamana
(ii)
Uongozi ni dhima
(iii)
Uongozi ni amanah.
Pamoja
na hayo, kutokuwa na uongozi ni kujikaribisha kwa shaitwan.
Al- hadith
Kila
mmoja wenu ni mchunga na kila mcunga ataulizwa
juu ya kile alichokichunga [4]
Tukiitafakari hadithi hii kwa kina , tunajifunza
kuwa pamoja na kuwa na uongozi, wanaoongozwa pia, wanalo jukumu la kuhakiisha
kuwa hakuna uongozi mbovu watu wajue kuwa wataulizwa juu ya
walichokidhunga. Iwapo ummah, Jumuiya,
taasisi au asasi itakuwa na uongozi mbovu, kila mwanjumuiya atakuwa masulia.
3.3 Dhima ya Uongozi
Dkt.
Jamal Badawi, profesa na mwenyeit wa menejiment na stratejia, katia Chuo kiku
cha
(i)
Utumishi kwa anaowaongoza.
(ii)
Ulinzi wa wafuasi dhidi ya ukandamizaji
Dhima
hii nayo imesisitizwa na mtume (s.a.w). kwamba
kiongozi anapaswa kuwalinda wafuasi wake dhidi ya ukatili uonezi na
ukandamizaji vile vile kiongozi anapaswa kuwezesha umaizi kuhusu Mungu , taqwa
na haki.[7]
(iii)
Ulezi wa wafuasi
Dhima
nyingine muhimu ni ulezi. Ukiwa kiongozi
unailea jumuiya, unawalea wafuasi, unailea
taasisi, unailea asasi. Jukumu la ulezi ni muhimu
4.0 MADARAKA YA KIONGOZI
Dhana
ya madaraka katika muktadha huu ni uwezo wa kupanga, kuratibu, tumia rasilimali
watu, taarifa au habari, na fedha, kufanya
mambo ya jumuiya, taasisi au asasi, yaene
4.1 Madaraka
kutokana na wadhifa (Legistrate
power)
Madaraka
aliyonayo mtu kutokna na wadhifa katika taasisi. Kwa ujumla uislam haupendekezi
waislam kuwa na uamilifu wa kampeni ya kuwatafuta nafasi ya mamlaka. Kwa
muislam kufanya kampeni ili apate wadhifa ambao utampa kampeni ili apate
wadhifa ambao utampa madaraka, ni ishara ya kuwa mtu huyo anatamaa ya wadhifa
kwa maslahi yake binafsi.
Al- hadith
Usiombe uongozi kwa sababu
utakapopewa uongozi
kutokana na kuomba, utaachiwa
pekee yako (bila msaada
wa Allah kutekeleza jukumu na wajibu
unaonasibiana nao)
Na kama umepewa uongozi bila
kuomba, utasaidiwa
(Na Allah katika utekelezaji wa majukumu
yako).[9]
4.2 Madaraka kutokana na uwezo wa kuzawadia.
Kiongozi
ambaye anatawala rasilimali za ummah, jamii au taasisi, anaweza pia kuwa na
uwezo wa kuzawadia kutokana na mamlaka na wajibu wkae. Maelezo haya ni sahihi pia katika mafundisho ya
uislam.[10]
Inapendeza kusikia kuwa Seyyid na Umar Ibn Khatb[11]
(r.q) alikuw aakiwalipa mishahara ya juu, maadisa wa dola ya kiislam. Alifanya
hivyo ili kuhakikisha kuwa hawashawishiki kupokea rushwa. Kwa kuwajali
aliwateua
Matumizi
sahihi ya madaraka haya yanawezesha mafanikio na uamilifu wa jumuiya na taasisi
au asasi za kiislamu
4.3 Madaraka ya kinguvu (Coeraive power)
Kwa
kuwa na mamlaka ya kiuonogzi, kiongozi anao uwezo wa kuadhibu kwa niaba ya
anaowaongoza na pia kwa maslahi ya anaowaongoza. Uislamu unatambua kuswihi kwa madaraka
haya, lakini unafundisha kuwa madaraka haya yasitumike kuwafanya wafuasi
kufanya uovu. Ni kwa ukweli huu Mtume (s.a.w) anayesema kuwa Utii (kwa
kiongozi) unatakiwa kwa lile tu lililo jema.[12]
Katika kusisitiza dhima ya kiongozi wa kiislam na matumizi mazuri ya madaraka
ya kinguvu, seyydina Umar (r.a) alinukuliwa akiwaambia watu:
Nimekuteulieni
magavana na mawakala, siyo kuwaadhibu au
kuchukua
fedha zetu bali kuwfundisha na kuwatumika. [13]
4.4 Madaraka kwa utaalamu (Expart power)
Kwa
kawaida kiongozi mwenye uelewa, maarfia, ujuzi na habari au taarifa muhimu,
anayo madaraka kitaalamu. Anao uwezo wa kuwafanya wafuasi watekeleze jukumu fulani
kwa mpangilio mzuri na kwa namna sahihi pasipo vikwazo.
Mfano:-
Katika
swala ya Jumaa mtu anapaswa kuchaguliwa kuwaongoza wanaosali, kwa kigezo cha
ujuzi na maarifa yake juu ya swala. Kutokana na utaalam alionao imam, maamuma
watamfuata katika utartibu mzima wa swala. Uwezo huu alionao Imam katika
wafanya maamuma wafuate ni madaraka kwa utaalamu juu ya swala.
Mfano
mwingine ni juu ya uweo wa Amir wa Daawah kuwafanya wanajumuiya kufuata maelezo
yake kutokana na hakika kuwa Amir huyo anayo maarifa juu ya
5.0 MISINGI YA MAADILI YA UONGOZI WA KIISLAM
Kwa
sababu kuongoza ni kutekeleza maamrisho ya Allah(s.w) na mafundisho ya mutume
(s.a.w) na kwa kuwa kuongoza pia ni kufanya ibada, basi kiongozi anapaswa
kutekeleza majukumu na wjaibu wa
maelekezo ya Quran na Sunnah pamoja na
kujikita katika Akhlaq ya kiislam (Islamic Moral character). Akhlaq ya Kiislam
inakuwa madhubuti kadiri mja anavyoongeza uthabiti katika kumuamini Mwenyezi
Mungu kupitia hatua nne za kiroho.
5.1 Iman
Ni
kuamini kwa dhati juu ya kuwa mwenyezi Mungu ni momoja ( Tawhid). Kwa kuwa na Imani, kiongozi atajielewa kuwa yeye na
vilivyo chini yake, vinamilikiwa na
Allah(S.w). Pia Iman inamkumbusha kiongozi juu ya akhera na umasuulia (Accoutability). Kwa hiyo Iman inamkumbusha kiongozi kuwajibika. Katika
kukazia hili, Quran imetaja na kuhusianisha Iman na amali njema si chini ya
mara 60[14]
Mfano
wa Sahaba, Amr Ibn Al Aas, aliteuliwa na mtume (s.a.w) katika uongozi, takriban
miezi mine tu baada ya kuingia katika uislam. Habari hii inaweza kuthibitishwa
kwa akusoma kitabu kilichoandikwa na Ibn Taymiyya kiitwacho ASSIYAH ASH- SHAR IYYA.
5.2 Islam
Ni
sehemu muhimu pia katika haiba na maadili ya kiongozi wa kiislamu. Isam hapa inamaana kujisalimisha kwa mwenyezi Mungu na pia kuwa na amani baina ya
mja na viumbe wa Allah (s.w), kwa njia ya kunyenyekea kwa Allah.[15]
Iman
ni mbegu na Islam ni mafanikio ya Iman.[16]
Kiongozi
mwenye Iman anapotekeleza jukumu la uongozi wake katika uislam, hathubutu
kujitukuza wala hatajaribu kujiona kuwa mbora zaidi ya wote na kila kitu.
Imam
Ali Ibn Abutalib (r.a) aliandika barua kwa Malik al Ashtar an Nukai, gavana mpya wa Misri
akishadidisha hoja hii.
Malik; unalazimika kutosahau kwamba
mtawala/ kionogzi wao, basi khalifa ni
kiongozi wako
na mwenyezi Mungu ni juu ya khalifa.[17]
5.3 Taqwa
Hii
ni hisia ya heshima na uelewa vikichanganyika na kumuogopa Mwenyezi Mungu. Kwa
kuwa na Taqwa, kiongozi anakuwa na umaizi (consciousness) kuhusu jukumu
Msingi
wa taqwa upo katika mtizamo w amoyo na akili
kuliko
muonekano wa nje.
Kwa
hiyo taqwa inamfanya kiongozi anakuwa na mkao wa akili, fikra, hisa na maono
yanayoakisi uislam. Kwa sababu hiyo, uongozi wa kiongozi huyo utaendana na
amali njema.
kwa
hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na
kufanya hisani, na kuwapa
jamaa (na wengineo): na
anakataza uchafu na uovu na dhuluma.
Anakunasihini
ili mpate kufahamu (mfuate). (An nahl)[18]
5.4 Ihsan
Wakati
taqwa inahusisha kumwoogopa Allah (sw) na kuwa na hisa juu ya kuwepo kwake,
Ihsan ni Kumpenda Mwenyezi Mungu. Ihsani inamfanya kiongozi kuwa na juhudi
katika kumridhisha Allah. Jitiahda hii itamfanya kiongozi kutekeleza wajibu wake
ipasavyo na kuifanya taasisi au Jumuiya ya kiislam kufanikiwa kwa kufuata misingi
ya Quran na Sunnah.
Al- hadith
Ihsan ni kumwabudu Mwenyezi Mungu kana kwmba
Unamwona. na
Kujaalia
kuwa anakutazama.[19]
Kiongozi
kuwa na Ihsan, ataongoza kwa uadilifu na kwa dhamira stahiki, mambo ambayo
yatawezesha ufanisi wa Jumuiya na mafanikio
ya jumuiya kwa ujumla kwa mnasaba wa madhumuni ya jumuiya na Taasisi ya
kiislam.
6.0 WASIFU WA KIONGOZI WA KIISLAM
6.1 Elimu na Hikmah
Ee
Mola wetu! Waletee Mtume anayetokana na wao, awasomee
Aya zako na kuwafundiaha kitabu (chako) na
hikma (nyingine)
na wafundishe kujitakasa (na kila mabaya)
(Al- Baqara, 2:129 )
Mfano wa wale waliopewa Taurati, kisha hawa
kuichukua
(kutumia) ni
nafuu kwavyo). Ni m- baya kabisa mfano wa watu waliozikadhibisha
Aya za MwenyeziMungu; na Mwenyezi Mungu hawaogopi
madhalimu (AL- Jumla, 62:05)
Aya
hizi zinaonyesha umuhimu wa Elimu na Hekma kwa kiongozi vinginevyo kiongozi
huyo ni sawa na punda aliyebeba vitabu. Aidha katika aya hizo na nyingine
kadha, zinaonesha kuwa Mtume (s.a.w) alipewa maarifa na hekmah ili aweze
kufanikisha mafundisho ya uislam katika ummah waka. Mazingatio tunayopata hapa
ni kuwa: kwa kuwa kiongozi wa kiislam anao wajibu kwa ummah, matumzi ya hekma
ni muhimu. Kiongozi anapaswa kutumia vema madaraka yake katika kufanya maamuzi
yanayoathiri jumuiya, jamii, ummah na taasisi, maamuzi ya kiongozi yafanywe kwa
hekma.
Kuna
mifano mingi katika Seerah ya Mtume (s.a.w) ambapo hekma yake ilizaa matunda
japokuwa baadhi ya masahabaa hawakuwa wameweza kuigundua mapema . Mfano mzuri
wa hoja hii unadhihiri katika mkataba wa Hudaibiyya mwaka wa 6 Hijiria[20]
6.2 Adl na Rahma
Adl na Rahmah ni mambo mawili muhimu
Adl bila Rahmah husababisha ukatili
wakati Rahmah bila Adl huzaa
mkanganyiko na
Mkorogo (disorder) [21]
Kiongozi anapaswa kuwa na sifa ya kuwezesha
msawezo (balance) makinifu baina ya mambo hayo mawili.
Enyi
mlioamini kuweni wasimamizi (wa kupitisha haki) kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu, muwe mkiota Shahada kwa
uadilifu.. (Al- Maidah, 5:08)
Enyi
mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu mtoapo ushahidi
kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu; japokuwa ni juu ya nafsi zenu, au juu ya
wazazi
(wenu) na jamaa (zenu).. (An
Nisaa, 4:135)
Kwa
kuzingatia mafundisho ya uislam, uadilifu ni kanuni inayopaswa kuongoza
mwenendo wa muislamu. Kwa kiongozi wa kiislam, kanuni hii ni ya muhimu zaidi
kutokana na wajibu alionao kwa taasisi, jumuiya, asasi, ummah na watu wanaowaongoza.
Pasipo kanuni hii, uonogzi wa kiongozi
utaingia dosari kubwa kitu ambacho kitzaa mdororo wa uonogozi
6.3 Ushujaa
na Ujasiri
Viongozi
wanaposwa kuwa mfano kwa kudhihirisha ushujaa na ujasiri. Kiongozi hapaswi
kuogopa kuikabili hatari. Ushujaa na ujasiri ni wasifu muhimu kwa kiongozi ili
aweze kuwawezesha wafuasi wake kutekeleza jukumu lao hususan linapokuwa ni
jukumu zito.
Mfano:
katika vita vya Badr ushujaa na ujasiri wa Amir Jeshi, ni miongoni mwa mambo
yaliyowezesha ushindi wa waislam katika viwanja vya Badr.
Wakati
tawi linapokuwa likikabiliana na changamoto kadhaa zikiwemo njama dhidi ya
Jumuiya ya kiislamu, ushujaa na ujasiri wa kiongozi ni miongoni mwa mambo
muhimu kwa ajili ya tawi
6.4
Uamuzi na Kuazimia
Kiongozi
lazima asiwe mzito kutoa maamuzi iwapo kiongozi ni mzito kuamua, ataiweka
taasisi, asasi au jumuiya anayoiongoza, katika hatari ya kuhasirika na
kudorora.
Uamuzi
unaocheleweshwa unaweza kuwa fursa ya kuhasirika.
(Zatar Bangash).
Mtume
(s.a.w) hakuwa mzito kuamua hata wakati alipokuwa katika hali nzito. Mathalani:
alikuwa mchukua uamuzi kwa wakati aliposhughulikia Banu Qaiynuka, Banu Nadhir
na Banu Quraidha makabila haya yalikuwa na chokochoko na vitimbi dhidi ya
Uislam na dola ya Kiislam.
6.5 Udhihirishaji dhamira
Kiongozi
lazima aweze kudhihirisha dhamira yake. Hii ni pamoja na kuweza kuonyesha
dhamira waziwazi na kuwavuta pamoja na kuwavuta watu katika dhamira hiyo kwa
kuzingaia seerah ya Mtume (s.a.w) mara tu alipoanza kuutangaza uislam, alibainisha
dhamira na kufanikiwa kuwavuta watu katika uislam mara moja. Hata wakati
makafiri wa kiquraish walipomtuma Utbah Ibn Rabah kumpelekea Mtume (s.a.w) machaguo
manne, ili kumfanya aache kuutangaza uislam, Mtume (s.a.w) alimsomea Utbah
sura ya Ha mim sajda, (sura ya 41 ). Katika kukataa pendekezo la makafiri, Mtume
(s.a.w) alifahamu kabisa kuwa uamuzi huo ungeongeza madhila kwa waislam, lakini aliona pia kuwa
kudhihirisha dhamira ilikuwa ni bora zaidi ya kutoridhisha. Kwamba kwa kutodhihirisha
dhamira ingekuwa haifai, haifai hasa. Ni
kwa mantiki hiyo hiyo, pindi viongozi wa TAMSA mashuleni na vyoni wanapopewa
maelekezo kutoka utawala, ambayo yanakinzana na matakwa ya uislam, wanapswa
kudhihirisha kuwa
7.0 UHUSIANO WA KIUTAWALA BAINA YA KIONGOZI
NA WAFUASI
Ingawa
kwa wakati wa sasa, Jumuiya na taasisi za kiislamu zina viongozi wanaitwa kwa
vyeo vizuri
7.1
Utii
Suala
muhimu la kuzingatia ni kwamba,
Utii
wa muislam kwa kiongozi wake ni amri ya mwenyezi Mungu.
Enyi
mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, Mtiini Mutume
wake(s.a.w)
na wale walio na mamlaka miongoni mwenu (Q.4:59)
Mtume
(s.a.w) amesisitiza
Yeyote anayenitii mimi, anamtii Allah (sw)
na yeyote asiyenitii mimi
hamtii Allah (sw) na
yeyote anayemtii kiongozi, ananitii mimi, na yeyote
asiyetii kiongozi basi
hanitii mimi[22]
Kwa
kuzingatia Quran na Sunnah kama ilivyoelezwa hapo ju, basi kielelezo cha
mamlaka na utii kinaweza kuwa
Kielelezo cha mtitiriko katika utii
MTUME KIONGOZI WAFUASI


![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Chanzo: Ufafanuzi wa mwandishi.
Mtume
(s.a.w) alisema pia:
Kusikia na kutii ni
jukumu la muislamu kwa yeyote
anayopenda na asiyoyapenda[23]
Uislam
umehimiza
7.1.1 Mipaka ya utii.
Pamoja na msisitizo juu ya utii kwa viongozi
lakini pia uislam haukubali utii wa
kibubusa.[24]
Dkt
Badawi na Dkt Beekun walipiga mfano wa tukio ambapo Seyydna Umar (r.a)
alipendekeza kiasi cha mahari kiwekwe maalum katika harusi. Kiasi alichokisema
hakikuwa kikiendana na sheria ya kiislam. Ukht mmoja akasimama na kumwambia. Umar muogope mwenyezi Mungu. Aliposikia
hoja nzuri iliyoendana na Quran na
Sunnah, Umar alibaini kosa lake na kusema kuwa ukht alikuwa sahihi, na tabia
hii ya Umar ni kielelezo kwamba wafuasi hawapaswi, kupokea maelekezo ya kiongozi pasipo kutafakari, na pale ambapo wafuasi
wanaona kiongozi amekosea, wanapaswa kumkosoa.
Mipaka ya utii ni pamoja na hii ifuatayo:-
(i)
Kutowatii
maasi
Wala
msitii amri za wale maasi (Q.21:151)
Ambao wanafanya uharibifu tu katika ardhi
wala hawaitengenezi (Q.26:152)
(ii)
Hakuna
utii wa kutokutii
Imam Ali (r.a) amesema:
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alituma skauti
na kumfanya mmoja wa Ansar kuwa kiongozi. Akawataka wamtii na kumsikiliza.
Haraka wakamuudhi kiongozi wao, naye akawaamrisha kukusanya kuni na kuzitia
moto, kisha akawaambia, hamkuambiwa na mtume (s.a.w) kumtii na kunisikiliza?
Wakasema Ndiyo! Kisha akawaamrisha waingie kwenye moto; wakakataa kuingia kwenye moto. Walioporudi
walimweleza mtume (s.a.w) kilichotokea,
naye akawaambia kuwa laiti wangeliingia kwenye moto wasingetoka tena.
Haiwzekani kuwepo utii wa kutokutii[25]
Hata
katika swala za jamaa,
Baada ya kuona mipaka ya utii, suala linakuja
:utii ni kwa nani?
Al- hadith
Msikilizeni na mtiini hata
8.0 HITIMISHO
Tuongoze njia
iliyonyooka, njia ya wale uliowaneemekea, sio ya wale
uliowaghadhibikia, wala wale
waliopotea.. (Q. 1:50-6)
Ni
jukumu letu waislam, ni jukumu la viongozi wa waislam kutafuta njia iliyonyooka
na kuifuata. Kuhusu sanaa na mchakto wa
uongozi, ipo njia iliyonyooka ambayo tunapaswa kuifuata sote.
Mafunzo
yoyote, yawe Bungua bongo, darasa duara, semina au warsha yanapaswa
kuwabadilisha watu katika mwelekeo (A), Stadi(s), maarifa (K) na uzoefu (E).
Viongozi waliokutana leo wanapaswa
kujiuliza jipya walilopata katika shughuli hii. Tuendapo tukazingatie pamoja na
mambo mengine, hatua zifuatazo baada ya
nukuu hii.
Kiongozi
atakayeweza kufanikiwa ni yule atakayefikia malengo kwa
namna nzuri
iwezekanayo, ikiwa ni kwa kiwango chini
kabisa cha
kutokuwa na ufaaji kwa
anaowaongoza, tena kwa gharama za chini kabisa,
kwa wakati muafaka na kwa viwango bora vya
utendaji (Abdul Ghani
Ahmed)[27]
Pamoja
na mbinu za kisasa za uongozi, kuna namna nyingi ya kuliendea
Kwa
hakika kutoka kwa mtume wa allah mnamfano wa kiga (Q.33:21)
Kwa
hiyo kiongozi azingatie
Mwenye uthabiti/ nguvu si yule ambaye
anawashinga wenzaka
kwa maguvu ila ni yule ambaye ingawa amekasirka,
anajidhibiti.[28]
Liwepo
katika ninyi kundi ambalo litawalinganisa watu kufanya
mema,
kusimamisha haki na kukataza mabaya. Watu hao ndio
watakaofanikiwa (Q.3:104)
Wale ambao kwa imani kubwa wanatunza
uaminifu wao naahadi zao
ndo watu wa peponi; humo watakaa milele. (Q. 23:8)
Tuliwatuma mitume wetu pamoja na kuwapa
mwongozo na vitabu na
vipimo vya ili wapate
kusimamia uadilif (Q.57:25)
Mtu
atakamilika katika dini yake (Islam) pale ambapo ataacha
lisilomuhusu. (Tirmidh)[29]
Enyi
miloamini mfuateni Mwenyezi Mungu na muwe pamoja na
wakweli (Q. 9:119)
Kuna
ishara 3 za mnafiki. Akisema anadaganya; akiahidi hatizimizi;
akiaminiwa husaliti
uamini (Imesimuliwa
na Abu Huraira (n.q) [30]
Kila shughuli isiyoanza kwa kumtakasa Allah(s.w)
haitofanikiwa
(Abu
Dawud)[31]
Kila
mmoja wenu ni mwangalizi na anawajibika juu ya waliochini ya
mamlaka yake. Mtawala ni mwangalizi na hivyo
anao wajibu juu ya
waliochini
yake. Mwanamume anaowajibu juu ya familia yake na wote
walio chinni ya uangalizi wake kwa namna hiyo
hiyo kila mmoja wenu
ni mwangalizi na mwenye wajibi kwa dhamana
aliyonayo.[32]
Hamtafikia
uchamungu mpaka mtoe katika mnavyovipenda.
Na chochote
manachotumia Mwenyezi Mungu anafahamu (Q. 3:92)
Na
shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala
msifarakane; na kumbukeni neema ya Mwenyezi
Mungu iliyo juu
yenu
mlipokuwa maadaui, naye akaziunganisha nyoyo
zenu, hivyo
kwa neema yake mkawa ndugu; na mlikuwa
ukingoni mwa shimo la
moto
naye akawaokoeni. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu
anavyokubainishieni
Aya zake ili mpate kuongoka. (Q. 3:103) [33]
Wakati
watu watatu wanondoka kwenda safari, wamchague
mmoja wao kuwa kiongozi[34]
12. Kuwa katika Timu
Waumini
wa kweli miongoni mwao ni
zinakamatana na kushikamana hasa kila moja,
aliposema hivyo
Mtume (s.a.w) alishikamanisha vidole
vya mikono yake (Interlocking)[35]
MWISHO
WA
BILLAH TAWFIQ
ALLAH
NDIYE MJUZI WA YOTE
[1] Tanzania Problems faced by Dawah and
the D aiyah, uk.77
[2] Fasiri iliyotolewa
[3] Taz. Training Guide for Islamic
workers, Dkt. Hisham (1993)
[4] Taz.
Sunnah al Tirmith, Sunnah Abu Dawud, Sahili al Muslim, Sahih al Bukhar.
[5] Taz.Omar Hassan Kasule, Sr. Leadership
Module, General theme: Leadership. Workship 1. In muslim leaders forum 98
Handbook. (
[6] Taz. Mwito kwa waislamu kuimarisha
umoja wao Mwinyi, 1988, uk.10
[7] Taz. The leadership process in Islam,
Beekun and Badawi,
[8]
Taz. Beekun and Badawi (1999) the leadership process in Islam, p.3
[9] Badawi Anarejea sahihi Muslim, volume
3, 1013.
[10] Taz. Dkt. Badawi (k.h.j.)
[11] Khalifa wa pila katika Uislam
[12] Sahihi Bukhar, volume 9, hadith 259,
sahihi Bukhar vol. 5, hadith 629
[13] Taz. Muhammad Al Buraey.
Administrative development: An Islamic perspective (London , U.K.: KPI,
1985),248
[14] Imeelezwa hivyo na Dkt Badawi katika
makala aliyoandika kwa kushirikiana na Dkt Beekun, 1999
[15] Naceur Jabnourn, Islam and Management,
1994
[16] Taz. Sayyid Abu A la maudodi: The Islamic movement: dynamics
of values, power and change .
[17] Taz. Behzadnia and Denny: To the
commander in chief: form Iman Ali to malik E- Ashter (1981)p.8
[18] Quran sura ya 16 aya ya 90
[19] Nukuu ya Dkt Badawi, ni Sahihi Muslim,
hadith 1:47
[20] Taz. http://www.
Islamicthought. Org/ pp- 26 leader. Html. The Concept of leader and
leadership by Zafar Bangash.
[21] Taz. Zafar Bangash, (khj,
[22] Taz. Al Bukhar na Muslim
[23] Amesimulia Ibn Umar, tazama Rahman, 75
[24] Taz. Badawi and Beekun (1999) The
leadership process in Islam,
[25] Taz. Fathi Yakan, problems facing da
awah and daiyah,
[26] Sahihi Muslim na Sahih Bukhar
[27] Taz. A Z steps to leadership in
Islam, htt://www. Geocities.com multmainaa/takkur/leadership
Islamic htm/?2006 24/4/2006
[28] Hadith kutoka sahihi al Bukhar
[29] Imenukuliwa na Abdul Ghani Ahamed
Barrie (khj)
[30] Khj
[31] Tafsiri ya mwandishi, kutoka khj
[32] Taz. Htt:/ www. Geocities.
Com/mutmainaa/tafakkr/leadership- Islam. Html? 2000624
[33] Khj
[34] Taz. Dibaji iliyoandikwa na Sheikh
Ramadhan Tahir Mpendu wa BALUKTA
3/9/1988 Mwito Kwa Waislam Kuimarisha Umoja Wao
[35] Abdul Ghani anarejea shih al Bukhar